Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Job Sikhala, mpinzani wa Zimbabwe, ataachiliwa kutoka jela

Job Sikhala, kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, ataachiliwa hivi karibuni baada ya zaidi ya mwaka mmoja na nusu kuzuiliwa katika gereza lenye ulinzi mkali katika mji mkuu wa Harare, wakili wake Harrison Nkomo ametangaza siku ya Jumanne.

Aliyekuwa mbunge wa Zimbabwe na mwanachama maarufu wa chama cha upinzani cha Citizens Coalition for Change (CCC) Job Sikhala akisalimiana na waandishi wa habari na wafuasi wake nje ya Mahakama ya Harare Januari 24, 2024.
Aliyekuwa mbunge wa Zimbabwe na mwanachama maarufu wa chama cha upinzani cha Citizens Coalition for Change (CCC) Job Sikhala akisalimiana na waandishi wa habari na wafuasi wake nje ya Mahakama ya Harare Januari 24, 2024. © Jekesai NJIKIZANA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Alipopatikana na hatia ya kuchochea ghasia wiki jana, mpinzani huyo mwenye umri wa miaka 51 alihukumiwa Jumanne na mahakama kifungo cha miaka miwili jela. "Sasa ni mtu huru. Hii ndiyo kesi pekee iliyomfanya ashikwe gerezani, hivyo ataachiliwa huru," Nkomo amewaambia waandishi wa habari baada ya kusikilizwa katika mahakama ya Harare.

Katika tangazo la kuachiliwa kwake katika siku zijazo, wafuasi kadhaa waliimba na kuinua ngumi zao kwa ushindi kwenye ngazi za mahakama. Bw. Sikhala, mwanasheria na mtu mwenye mvuto anayependwa na watu wa hali ya chini wa Harare, alifunguliwa mashitaka katika kesi hii na mbunge wa upinzani, Godfrey Sithole. Mbunge huyu wa upinzani pia alipatikana na hatia na akapewa hukumu kama hiyo, kufuatia kesi hii iliyochukua muda wa mwaka mmoja.

Mamlaka iliwashutumu watu hao wawili kwa kuwachochea wanachama wa Chama cha Wananchi kwa ajili ya Mabadiliko (CCC), chama kikuu cha upinzani, kulipiza kisasi kifo cha mwanaharakati, Moreblessing Ali, ambaye mwili wake uliokatwakatwa ulipatikana kisimani mwezi Mei 2022. Mahakama ilisema kuwa watu hao wawili walichochea ghasia za umma kwa kuwasafirisha waombolezaji hadi kwenye sherehe za ukumbusho wa Bi Ali, ambazo zilikumbwa na ghasia.

Job Sikhala aliwakilisha familia ya mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 46 aliyeuawa baada ya kutekwa nyara na mwanaharakati wa chama tawala cha Zanu-PF. Akiwa kizuizini tangu mwezi Juni 2022, anasubiri uamuzi katika kesi nyingine mbili, "zinazochochewa kisiasa" kulingana na wafuasi wake, lakini aliachiliwa kwa dhamana katika muktadha wa kesi hizi. Hasa anashitakiwa kwa kuchapisha habari za uongo.

Chama cha Zanu-PF, kikiwa madarakani tangu uhuru mwaka 1980, kinashutumiwa kwa kuongoza kampeni kubwa ya vitisho dhidi ya wapinzani wake. Mnamo mwezi Agosti, uchaguzi uliokumbwa na ushindani ulipelekea kuchaguliwa tena kwa Rais Emmerson Mnangagwa, 81, kama mkuu wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.