Pata taarifa kuu
SIASA-USALAMA

Zimbabwe: Nelson ajiondoa katika chama kikuu cha upinzani cha CCC

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa, mgombea ambaye aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Agosti mwaka jana, ametangaza siku ya Alhamisi kwamba anakihama chama chake "kilichochafuliwa, kimeibiwa na kutekwa nyara" na utawala unaotumia "vitisho na vurugu" kwa wapinzani na raia.

Kiongozi wa upinzaji nchini Zimbabwe Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari.
Kiongozi wa upinzaji nchini Zimbabwe Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

 

"Mara moja, sina uhusiano tena na CCC," Muungano wa Citizens for Change, chama kikuu cha upinzani nchini humo, amesema mpinzani huyo, mwanasheria na mchungaji mwenye umri wa miaka 45, katika taarifa yake. Amesema atawafahamisha Wazimbabwe kuhusu mipango yake ya siku za usoni, bila kufichua chochote katika hatua hii.

"CCC imekuwa tawi la chama cha Zanu-PF, ambacho kinalidhibiti," amesema Bw. Chamisa, akiongeza bila kutoa maelezo kwamba chama chake "kimechafuliwa, kiimeibiwa na kutekwa nyara" na chama tawala cha rais Emmerson Mnangagwa. "Ninakataa kuogelea kwenye mto wenye mamba wenye njaa," amesema.

Emmerson Mnangagwa, 81, aliyepewa jina la utani la "mamba" kwa sifa yake kama rais wa kimabavu, alichaguliwa tena mwezi Agosti 2023 kama mkuu wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika. Emmerson Mnangagwa ambaye anashutumiwa kwa utawala wa kiimla uliopindukia na kuongoza kampeni kubwa ya vitisho dhidi ya wapinzani wake, alimrithi Robert Mugabe, aliyeondolewa madarakani mwaka 2017, kupitia mapinduzi.

Upinzani ulishutumu "uchaguzi uliokumbwa na kasoro" mnamo mwezi Agosti na kudai ushindi. Waangalizi wa kimataifa waliripoti ukiukaji wa "kanuni nyingi za kimataifa".

Akikumbusha "unyanyasaji wa ajabu na usio na aibu tuliofanyiwa wakati wa kampeni" na "vitisho na ghasia zilizofanywa kwa raia wa Zimbabwe wakati na baada ya uchaguzi", Nelson Chamisa ameonya dhidi ya "rais aliye madarakani (ambaye) anataka upinzani kudhibitiwa na serikali."

Wakati wa kampeni za uchaguzi, mikutano mingi ya upinzani ilipigwa marufuku na wapinzani kukamatwa. Kufuatia uchaguzi huo, takriban wabunge thelathini wa upinzani walifutwa kazi kwa sababu zisizoeleweka.

Katika miezi ya hivi karibuni, wanaharakati kadhaa wa upinzani wameshambuliwa, mmoja wao akipatikana amekufa baada ya kutekwa nyara. Zimbabwe inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi kwa takriban miaka ishirini. Nchi hii inalemewa na kasumba ya kukatika kwa umeme, uhaba na ukosefu wa ajira uliokithiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.