Pata taarifa kuu

UN yaeleza kuguswa na uchaguzi wa Zimbabwe

Nairobi – Katibu mkuu wa umoja wa mataifa António Guterres ameeleza wasiwasi wake kuhusu kukamatwa kwa waangalizi wa uchaguzi nchini  Zimbabwe wakati huu pia kukiwa na madai ya kutishwa na kuhangaishwa kwa wapiga kura.

Mpiga kura akishiriki zoezi la uchaguzi wa urais na wabunge jijini Harare, Tarehe 24 Agosti 2023.
Mpiga kura akishiriki zoezi la uchaguzi wa urais na wabunge jijini Harare, Tarehe 24 Agosti 2023. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa UN kupitia msemaji wake, ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa nchini humo na wafuasi wako kuepukana na njia zozote za uchochezi na kwamba kuna haja ya kuheshimiwa kwa haki za binadamu na sheria ya taifa hilo.

Tume ya uchaguzi nchini humo ilimtangaza rais Emmerson Mnangagwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kupata asilimia 52.6 ya kura zote zilizopigwa.

Rais wa Emmerson Mnangagwa ametangazwa mshindi wa uchaguzi huo
Rais wa Emmerson Mnangagwa ametangazwa mshindi wa uchaguzi huo AFP - JEKESAI NJIKIZANA

Licha ya tangazo hilo la tume ya uchaguzi, upinzani kwa upande wake unasema ulishinda katika uchaguzi huo, ukisema kulikuwepo na udaganyifu.Waanaglizi wa uchaguzi wamesema zoezi hilo halikuafikia vigezo wa kidemokrasia.

Wiki iliyopita, zaidi ya waangalizi 40 walikamatwa wakijaribu kuainisha matokeo yao na yale ya tume ya uchaguzi.

Kiongozi wa upinzaji nchini Zimbabwe Nelson Chamisa amepinga matokeo hayo
Kiongozi wa upinzaji nchini Zimbabwe Nelson Chamisa amepinga matokeo hayo REUTERS/Mike Hutchings

Hatua ya kukatwa kwao imekashifiwa vikali na makundi ya watetezi za haki za binadamu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.