Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Mwanasiasa wa upinzani atekwa nyara na kupatikana amefariki nchini Zimbabwe

Mwanaharakati wa upinzani nchini Zimbabwe amepatikana amekufa baada ya kutekwa nyara alipokuwa akifanya kampeni kabla ya uchaguzi mdogo, chama chake kimesema.

Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari huko Harare Julai 17, 2018.
Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari huko Harare Julai 17, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Hili ni tukio la tatu kushutumiwa ndani ya wiki chache na Chama cha Wananchi kwa ajili ya Mabadiliko (CCC), chama kikubwa cha upinzani nchini, ambacho kinakishutumu chama tawala, Zanu-PF, kwa kuongoza vitisho vikubwa vya kampeni dhidi ya wafuasi wake.

Mwishoni mwa mwezi Oktoba na mwanzoni mwa Novemba, CCC ilitangaza kuwa mmoja wa wabunge wake na mbunge wa zamani walitekwa nyara mjini Harare, waliteswa na kisha kupatikana wakiwa uchi. Siku ya Jumatatu CCC ilisema kwamba mwili wa Tapfumanei Masaya, aliyetekwa nyara mchana kweupe na watu wenye silaha Jumamosi iliyopita mjini Harare, umepatikana viungani mwa mji mkuu.

"Tunatoa wito kwa polisi kuchunguza uhalifu huu wa chuki na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria," chama hicho kilisema kwenye mtandao wa X (zamani ikiitwa Twitter). Polisi ilithibitisha kuwa mwili ulipatikana bila kuthibitisha utambulisho huo, ambao walisema bado haujafahamika.

Mnamo mwezi Agosti, uchaguzi uliokuwa na ushindani ulisababisha kuchaguliwa tena kwa Rais Emmerson Mnangagwa kama kiongozi wa nchi. Tangu wakati huo Bunge lilitangaza wazi viti vya wabuge15 waliochaguliwa wa chama cha CCC, ambacho kiilishutumu uamuzi wa "udanganyifu", na uchaguzi mdogo unapangwa mwezi Desemba ili kuzijazia nafasi hizo.

Tapfumanei Masaya alikuwa akimfanyia kampeni mgombea wa CCC huko Mabvuku, kitongoji cha Harare, alipolazimishwa kuingia kwenye gari, kulingana na chama chake. Kufutwa "kinyume cha sheria" na kwa uchaguzi wa wabunge wetu "kulisababisha kifo (chake)", iliandika CCC kwenye mitandao ya kijamii.

Mwezi Agosti, kiongozi wa CCC Nelson Chamisa, 45, alishindwa na Rais Mnangagwa, 81, katika uchaguzi mkuu ambao pia uliipa Zanu-PF kura nyingi bungeni. Kulingana na waangalizi wa kimataifa, uchaguzi huu haukuheshimu viwango vya kidemokrasia. Na uchaguzi mdogo ujao unaweza kuipa Zanu-PF, madarakani tangu uhuru mwaka 1980, thuluthi mbili ya wingi wa wabunge katika Bunge, muhimu ili kurekebisha Katiba.

Kulingana na baadhi ya wachambuzi, Zanu-PF inaweza kuchukua fursa hiyo kumruhusu Bw Mnangagwa, ambaye aliingia madarakani baada ya mapinduzi yaliyompindua rais Robert Mugabe mwaka wa 2017, kusalia madarakani baada ya mwaka 2028.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.