Pata taarifa kuu

Msumbiji: Watu 67,000 watoroka makazi yao baada ya mashambulizi ya hivi karibuni

Serikali ya Msumbiji iimetangaza Jumanne kwamba makumi ya maelfu ya watu wamelazimika kutoroka makaazi yao kutokana na wimbi la hivi karibuni la mashambulizi ya wanajihadi kaskazini mwa nchi hiyo, lakini imekataa kutangaza hali ya hatari.

Mlipuko mpya wa ghasia ulitokea kaskazini mwa Msumbiji takriban wiki mbili zilizopita, kulingana na vyanzo vya ndani na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), shirika la Umoja wa Mataifa.
Mlipuko mpya wa ghasia ulitokea kaskazini mwa Msumbiji takriban wiki mbili zilizopita, kulingana na vyanzo vya ndani na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), shirika la Umoja wa Mataifa. © MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tunazungumza kuhusu watu 67,321 waliokimbia makazi yao," msemaji wa serikali Filimao Suaze amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Maputo, akizungumzia hali katika jimbo la Cabo Delgado. Idadi hii, kulingana na Bw. Suaze, "inalingana na familia 14,270 ambazo kwa hivyo zinachukuliwa kuwa zimefika katika jimbo la Nampula na (...) maeneo mengine". Bw. Suaze ameongeza kuwa serikali "haiamini kwamba masharti muhimu ya kutangaza hali ya hatari (...) huko Cabo Delgado yanatimizwa kwa sasa."

Mlipuko mpya wa ghasia ulitokea kaskazini mwa Msumbiji takriban wiki mbili zilizopita, kulingana na vyanzo vya ndani na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), shirika la Umoja wa Mataifa. IOM inakadiria idadi ya watu waliotoroka makazi yao waliokimbia mashambulizi huko Macomia, Chiure, Mecufi, Mocimboa da Praia na Muidumbe kati ya Desemba 22 na Februari 25 ni watu 71,681.

Kati ya siku ya Jumatano ya wiki iliyopita na siku ya Alhamisi, IOM ilirekodi kuwasili kwa zaidi ya watu 30,000 waliokimbia makazi yao, kwa basi, boti au kwa miguu, huko Namapa, mji ulioko kusini mwa jimbo la Cabo Delgado. Mahitaji ya kimsingi yanahusu chakula, malazi kwa waliokimbia makazi yao na huduma za afya, msemaji wa IOM ameliambia shirika la habari la AFP.

Tangu mwaka wa 2017, jimbo la kaskazini lenye utajiri wa gesi la koloni la zamani la Ureno, karibu na mpaka wa Tanzania, limekuwa eneo la uasi unaoongozwa na wanajihadi wanaohusishwa na kundi la Islamic State (IS). Kwa msaada wa maelfu ya wanajeshi kutoka nchi jirani na Rwanda, serikali imepata tena udhibiti wa sehemu kubwa ya jimbo hilo lakini mashambulizi ya wanajihadi yanaendelea. Bw. Suaze amehakikisha kwamba Msumbiji "inafanya kila iwezalo" "kupambana na ugaidi na kuhakikisha usalama wa watu."

Wiki iliyopita, Rais Filipe Nyusi alithibitisha watu wameanza tena kutoroka makaazi yao lakini akathibitisha kuwa vikosi vya usalama vinadhibiti hali ya mambo. Takriban watu 5,000 wameuawa na milioni moja wametoroka makazi yao tangu kuanza kwa uasi wa wanajihadi huko Cabo Delgado.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.