Pata taarifa kuu

Msumbiji: Raia waliorejelea makazi yao wakabiliwa na uhaba wa chakula

Nairobi – Nchini Msumbiji, familia ambazo zimerejelea makazi yao katika eneo la kaskazini mwa taifa hilo baada ya kuyatoroka kwa hofu ya kushambuliwa na makundi ya watu wenye silaha wanasema hawana chakula.

Jimbo la Cabo Delgado limekuwa likikabiliwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa makundi yenye silaha
Jimbo la Cabo Delgado limekuwa likikabiliwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa makundi yenye silaha © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wakazi hao, shughuli za kilimo hazijafanywa katika wilaya ya Nangade na kwamba hawajapata usaidizi wowote kutoka kwa serikali wala mashirika ya misaada.

Wakazi hao wameeleza kuwa wanalazimika kula vyakula vya msituni kutokana na ukosefu huo wa chakula haswa wakati huu wanapojaribu kujitengenezea makazi mapya ya kuishi.

Nangade ni wilaya inayopatikana katika jimbo lenye utajiri wa gesi la Cabo Delgado, ambalo limekuwa likikabiliwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa makundi ya watu wenye silaha wanaotaka kujinufaisha na bidhaa za gesi. Makundi yenye silaha yamekuwa yakipambana na serikali tangu mwaka wa 2017.

Watu elfu nne wameripotiwa kufariki katika makabiliano hayo wakati wengine laki nane wakiwa wametoroka makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.