Pata taarifa kuu

Msumbiji: Chama tawala kimeshinda katika uchaguzi wa manispaa

Watu wawili wameuawa jijini Maputo nchini Msumbiji, baada ya waandamanaji kutoka vyama vya upinzani kukabiliana na polisi, wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa Manispaa, ambao upinzani ukiongozwa na chama kikuu cha upinzani RENAMO unasema, demokrasia nchini humo umeuliwa.

Raia wa Msumbiji wakijiandaa kupiga kura katika Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Majimbo wa nchi hiyo katika kituo cha kupigia kura mjini Maputo, Oktoba 28, 2009.
Raia wa Msumbiji wakijiandaa kupiga kura katika Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Majimbo wa nchi hiyo katika kituo cha kupigia kura mjini Maputo, Oktoba 28, 2009. Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

Wito huu wa upinzani umekuja baada ya Tume ya Uchaguzi kukitangaza chama tawala cha Frelimo, kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika Oktoba tarehe 11.

 

Siku ya Alhamisi, Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuwa chama hicho ambacho kimekuwa madarakani tangu  ilipopata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975, kilitangazwa mshindi kwa kupata viti 64 kati ya 65 kwenye miji ya nchi hiyo.

 

Vyama 21 ndivyo vilivyoshiriki kwenye uchaguzi huo, huku vile vya upinzani vikidai kuwa wizi wa kura, vikiungwa mkono na mashirika ya kiraia.

 

Kwa mujibu wa uchaguzi huo, chama cha RENAMO hakijapata kiti chochote katika uchaguzi huo, huku chama kingine cha upinzani cha MDM kikipata ushindi kwenye mji wa Beira.

 

Kabla ya uchaguzi huu, upinzani ulikuwa unaogoza katika miji saba likiwemo jiji kuu Maputo ambalo sasa upinzani hauna mwakilishi wowote.

 

Upinzani unasema matokeo ya uchaguzi huo ni kama mauaji ya demokrasia nchini Msumbiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.