Pata taarifa kuu

Uchaguzi mkuu kufanyika nchini Msumbiji tarehe tisa Oktoba 2024

Nairobi – Raia nchini Msumbiji watashiriki uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka ujao kuwachagua viongozi wao wapya, serikali katika taifa hilo lenye utajiri wa gesi, imekuwa ikikabiliana na makundi ya waasi kwa muda sasa.

Katiba ya taifa hilo haitoi nafasi kwa rais Nyusi mwenye umri wa miaka 64, kuwania kwa muhula wa tatu.
Katiba ya taifa hilo haitoi nafasi kwa rais Nyusi mwenye umri wa miaka 64, kuwania kwa muhula wa tatu. AFP - PHILL MAGAKOE
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura nchini humo wanatarajiwa kupiga kura kumchagua rais wao mpya na wabunge na viongozi wengine katika mikoa tarehe tisa ya mwezi Oktoba mwaka wa 2024.

Uamuzi huo umeafikiwa wakati wa kikao cha baraza la kitaifa chini ya uwenyekiti wa rais wa sasa Filipe Nyusi.

Katiba ya taifa hilo haitoi nafasi kwa rais Nyusi mwenye umri wa miaka 64, kuwania kwa muhula wa tatu.

Licha ya tangazo hilo, Chama cha Frelimo ambacho kimekuwa madarakani tangu taifa hilo kujipatia uhuru wake kutoka kwa Ureno mwaka wa 1975 hakijamchagua mgombea wake wa urais.

Frelimo kilishinda kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka wa 2019 baada ya kupata asilimia 73 ya kura zilizopigwa.

Chama cha upinzani cha Renamo, kiliputilia mabali ushindi huo kwa madai ya kukosa Imani na zoezi hilo.

Frelimo na Renamo zilipigana vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia 1975-1992, na kuharibu uchumi wa taifa hilo na kuacha karibu watu milioni moja wakiwa wamekufa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.