Pata taarifa kuu

Algeria: Waziri wa zamani Khaled Nezzar afariki dunia

Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Algeria Khaled Nezzar amefariki dunia mjini Algiers akiwa na umri wa miaka 86. Jenerali mstaafu, alikuwa anashukiwa kuratibu vitendo vya mateso dhidi ya wapinzani wa Kiislamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Algeria katika miaka ya 1990.

Picha iliyopigwa Januari 9, 2016 inamuonyesha aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Algeria, Khaled Nezzar akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Algiers.
Picha iliyopigwa Januari 9, 2016 inamuonyesha aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Algeria, Khaled Nezzar akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Algiers. AFP - RYAD KRAMDI
Matangazo ya kibiashara

Khaled Nezzar alikuwa anashitakiwa na mahakama ya Uswisi kwa "uhalifu wa kivita" na "uhalifu dhidi ya binadamu". Siku moja kabla ya kifo chake, mahakama ilitangaza kwamba kesi yake ingeanza Juni 2024.

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune alitoa rambirambi zake kwa "mmoja wa watu mashuhuri zaidi wa kijeshi" ambaye alijitolea maisha yake "kutumikia taifa".

Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Algeria aliashiria, kwa miaka mingi, sera ya usalama, hata ya ukandamizaji, ya serikali ya Algeria kutoka kwa uchaguzi wa wabunge wa mwaka 1991 ambao uliingiliwa na mamlaka. Chama cha Islamic Salvation Front (FIS) kilikuwa mbioni kushinda uchaguzi. Kisha nchi hiyo ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka kumi kati ya wanajeshi waliokuwa madarakani na wanamgambo wa Kiislam.

Kuanzia mwaka 1992 hadi mwaka 1994, alikuwa mmoja wa wajumbe watano wa Kamati Kuu ya nchi iliyoongozwa na Mohamed Boudiaf. Kisha alistaafu lakini alibaki kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya utawala, akihakikisha kwamba maslahi ya jeshi yanazingatiwa.

Alipokamatwa Geneva mwaka 2011, Mahakama ya Uswisi ilimshtaki rasmi miaka kumi na miwili baadaye. ilimtuhumu kwa kuunda miundo kwa kujua na kwa makusudi yenye lengo la kuangamiza upinzani wa Kiislamu.

Khaled Nezar ambaye alizaliwa mwaka wa 1937,  alitoka katika kizazi cha wapigania uhuru. Mnamo mwaka 1958, aliliacha jeshi la Ufaransa na kujiunga na Jeshi la Ukombozi la Kitaifa la Algeria. Mnamo mwezi Oktoba 1988, mkuu wa majeshi wakati huo, alikandamiza kwa umwagaji damu uasi wa watu wengi dhidi ya National Liberation Front . Takriban watu 500 waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.