Pata taarifa kuu

Niger : Algeria kuwa mpatanishi kusaidia kupata suluhu ya mzozo unaoendelea

Nairobi – Algeria, imesema utawala wa kijeshi nchini Niger, umekubali nchi hiyo kuwa mpatanishi kusaidia kupata suluhu ya mzozo unaoendelea baada ya mapinduzi dhidi ya rais Mohammed Bazoum, ambaye amefungua kesi dhidi ya wanajeshi hao kwenye mahakama ya ukanda.

Katika kuwasilisha mpango huo waziri wa mambo ya nje wa Algeria alizuru Nigeria, Benin na Ghana mataifa wanachama wa ECOWAS
Katika kuwasilisha mpango huo waziri wa mambo ya nje wa Algeria alizuru Nigeria, Benin na Ghana mataifa wanachama wa ECOWAS AP - Sam Mednick
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na wizara ya mambo ya nje, Algiers ilipokea taarifa ya kukubali upatanishi wa Algeria kutoka Niamey unaolenga kukuza suluhisho la kisiasa la mgogoro wa Niger ndani ya mfumo wa mpango wa suluhu uliowasilishwa na Rais Tebboune.

Kulingana na chanzo hicho hicho Ahmed Attaf, waziri wa mambo ya nje, hivi karibuni atasafiri hadi Niamey kuanza majadiliano ya maandalizi na washikadau wote kutekeleza mpango huu.

Raia wa Niger wamekuwa wakionekana kuunga mkono hatua ya jeshi kuchukua madaraka
Raia wa Niger wamekuwa wakionekana kuunga mkono hatua ya jeshi kuchukua madaraka © AFP

Pendekezo la Algeria lililowasilishwa na rais Abdelamadjid Tebboune tangu mwezi Agosti linaagiza mazungumzo ya kisiasa kwa ajili ya kurejea kwa utawala na wa kikatiba kwa kipindi cha miezi 6 chini ya kiongozi ataekubaliwa na washikadau wote.

Katika kuwasilisha mpango huo waziri wa mambo ya nje wa Algeria alizuru Nigeria, Benin na Ghana mataifa wanachama wa ECOWAS.

ECOWAS imekuwa ikitaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia
ECOWAS imekuwa ikitaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia REUTERS - FRANCIS KOKOROKO

Mwezi mmoja na nusu uliopita, Jenerali Tiani alizungumzia juu ya utawala wa mpito ambao haungeweza kuzidi miaka mitatu, mwelekeo ambao utawekwa kupitia mazungumzo ya kitaifa.

Hata hivyo upande wa ECOWAS wanasema hawajapokea ufafanuzi zaidi kuhusu juhudi hizi wa Algeria ambayo sio nchi mwanachama wa ECOWAS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.