Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa watoa wito kwa Algeria kuwaachilia huru watetezi wa haki za binadamu

Ripota wa Umoja wa Mataifa ametoa wito siku ya Jumanne kwa mamlaka ya Algeria kuwaachilia watetezi wote wa haki za binadamu wanaozuiliwa, baada ya kuzuru nchi hiyo.

"Sheria inayotumika kwa sasa inatumika kupunguza na kuidhinisha kazi ya watetezi wa haki za binadamu," analaani ripota wa Umoja wa Mataifa.
"Sheria inayotumika kwa sasa inatumika kupunguza na kuidhinisha kazi ya watetezi wa haki za binadamu," analaani ripota wa Umoja wa Mataifa. © AP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Algiers, Mary Lawlor, ripota maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu, ameitaka serikali ya Algeria "kuwaachilia watetezi wote wa haki za binadamu wanaozuiliwa kwa kutumia uhuru wao wa kujieleza, kutoa maoni na kujumuika.

Kulingana na Kamati ya Kitaifa ya kuachiliwa kwa Wafungwa (CNLD), makumi ya watu, wanaohusishwa na vuguvugu la kuunga mkono demokrasia la Hirak au utetezi wa uhuru wa mtu binafsi, bado wanazuiliwa nchini Algeria. Bi. Lawlor amedai kuwa amebainisha kupitia mahojiano aliyofanya wakati wa ziara yake "mifumo ya ukiukaji inayotumiwa kuwakandamiza" watetezi wa haki za binadamu, akitaja hasa "kuingiliwa kwa mahakama (...) kupitia mashtaka mengi ya jinai".

"Sheria inayotumika kwa sasa inatumika kuweka kikomo na kuidhinisha kazi ya watetezi wa haki za binadamu," aamesema Bi Lawlor, akibainisha matumizi ya kifungu cha kanuni ya adhabu inayohusishwa na masuala ya kigaidi ili "kuwakandamiza" wanaharakati hao. Kulingana naafisa huyo "ufafanuzi wa ugaidi katika kifungu hiki haueleweki na ni mpana sana hivi kwamba unaacha huduma za usalama na ujanja mkubwa wa kuwakamata watetezi wa haki za binadamu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.