Pata taarifa kuu

Algeria imechukua tahadhari kudhibiti msambao wa kunguni

Nairobi – Mamlaka nchini Algeria imeimarisha hatua za afya katika mipaka yake ili kupunguza kuenea kwa kunguni, ambao wameenea kote Ufaransa.

Ufaransa tayari imeanza kukabiliana na kunguni hao ambao wamezua wasiwasi ya kiafya
Ufaransa tayari imeanza kukabiliana na kunguni hao ambao wamezua wasiwasi ya kiafya REUTERS - STEPHANIE LECOCQ
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ilisema kuwa inaanzisha ufuatiliaji wa afya na kuua vijidudu kwa ndege, meli na magari katika sehemu za kuingilia.

Hii inakuja huku kukiwa na wasiwasi kwamba wadudu hao wanaonyonya damu wanaweza kuingia Algeria kutokana na idadi kubwa ya watu wanaosafiri kutoka Ufaransa.

Hata hivyo wizara hiyo imesema hakuna uvamizi wa kunguni ambao umeripotiwa nchini huku ikisisitiza kuwa makini.

Nchi jirani ya Morocco nayo pia tayari imetangaza mikakati ya kuzuia msambao wa wadudu hao katika eneo lake.

Masambao wa kunguni jijini Paris na miji mingine imezua wasiwasi nchini Ufaransa kuelekea mashindano ya Olimpki mwaka ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.