Pata taarifa kuu

Sahara Magharibi: Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa Morocco kuwaachilia wafungwa wa Sahrawi

"Morocco inapaswa kuwaachilia wafungwa wa kundi la Gdeim Izik": huu ni wito uliyotolewa na Jopo Kazi la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wanaozuiliwa holela (UNWGAD). Katika maoni ya tarehe 11 Oktoba, jopo hili lilihitimisha kuwa kuzuiliwa kwa wanaharakati kadhaa wa Sahrawi kwa miaka 13 katika magereza ya Morocco ni kinyume cha sheria.

Picha kutoka Novemba 9, 2010, wakati wa ikivunjwa kambi ya Gdeim Izik, karibu na Laayoune, katika Sahara Magharibi, na vikosi vya usalama vya Morocco, ambapo mamia ya watu walikamatwa.
Picha kutoka Novemba 9, 2010, wakati wa ikivunjwa kambi ya Gdeim Izik, karibu na Laayoune, katika Sahara Magharibi, na vikosi vya usalama vya Morocco, ambapo mamia ya watu walikamatwa. REUTERS/Handout/MAP
Matangazo ya kibiashara

Huu ni "ushindi mkubwa" kwa wanasheria na wanaharakati wa uhuru wa Sahara Magharibi, ambao sasa wanatoa wito kwa mamlaka ya Ufaransa kufanya kazi ili kuweza kuachiliwa kwao. Umoja wa Mataifa uliitaka Morocco, katika barua iliyoandikwa Oktoba 11, kuwaachilia huru waandamanaji wa Sahrawi, wanachama wa kundi linalojiita Gdeim Izik, ambao walipatikana na hatia ya mauaji ya askari wa vikosi vya usalama wakati mahakama za Morocco zilivunja kambi ya Gdeim Izik  mwaka 2013, na kufungwa tangu hapo.

Maoni haya kutoka kwa Jopo Kazi la Umoja wa Mataifa kuhusu kuwekwa kizuizini kiholela yanakaribishwa na Régine Villemont, kiongozi wa chama cha mshikamano na uungaji mkono wa kisiasa kwa Polisario (AARASD). "Ni kitu ambacho kilianza Oktoba na ambacho kilichukua muda kidogo kutoka kwenye bomba la Jopo Kazi, lakini ni kweli kwamba ni muhimu, kwa sababu bado ni msimamo unaochukuliwa hatua wazi na kali kwa upande wa Jopo Kazi, kutoka Geneva na Baraza la Haki za Kibinadamu, kwa njia fulani, kuifahamisha kwa uwazi Morocco kwamba wafungwa hawa wa Gdeim Izik walikamatwa chini ya mazingira yasiyo ya kawaida na waliteswa ili kukiri makosa ambayo hawakufanya,” amesema Régine.

"Kwa mara ya kwanza kulikuwa na kesi katika mahakama ya kijeshi, na rufaa, na yote haya katika hali ya kutofuata kanuni za sheria za kawaida za kuwekwa kizuizini kwa watu hawa 24. Zaidi ya hayo, walihukumiwa mwaka wa 2013 vifungo vizito sana, kifungo cha maisha jela, miaka 25, miaka 30… Ni karibu maisha yote,” ameongeza Régine Villemont.

Wasahrawi 24 walioshtakiwa walikuwa wamehukumiwa vifungo vya hadi maisha jela. Tayari wakati huo, watetezi wa haki za binadamu walikuwa wakipiga kelele kuhusu kesi ya kisiasa ya wanaharakati wa Sahrawi. Kufikia mwisho wa 2022, muungano wa mashirika na wanasheria walikuwa wamewasilisha malalamiko sita ya mateso dhidi ya Morocco kwenye kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya mateso, kwa niaba ya wafungwa sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.