Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Israel yatambua mamlaka ya Morocco kwa Sahara Magharibi

Tangazo hilo lilitolewa na baraza la mawaziri la kifalme huko Rabat, Jumatatu hii, Julai 17, jioni, kisha kuthibitishwa na serikali ya Israeli usiku. Ni katika barua iliyotumwa kwa Mfalme Mohamed VI, ambamo mambo makuu yalitangazwa, kwamba Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amerasimisha uamuzi huu wa kidiplomasia, miaka mitatu, baada ya kufufua uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Sahara Magharibi na majirani zake.
Sahara Magharibi na majirani zake. RFI
Matangazo ya kibiashara

Ni kupitia mitandao ya kijamii ambapo diplomasia ya Morocco ilirasimisha taarifa hizo: "Mfalme wake Mohammed VI amepokea barua kutoka kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ambaye amedhihirisha uungwaji wake mkono kwa Mfalme, uamuzi wa Serikali kwa Israeli kutambua uhuru wa Morocco kwaa eneo hilo la Sahara Magharibi".

Kisha inanyeshwa kwamba msimamo huu mpya wa kidiplomasia wa Israel"utaakisiwa katika vitendo vyote vya serikali ya Israel na kuwasilishwa mbele ya Umoja wa Mataifa" na kwamba "Israel inachunguza vyema kufunguliwa kwa ubalozi mdogo katika mji wa Dakhla", kusini-magharibi mwa eneo la Sahara Magharibi.

Huko Jerusalem, habari hii imethibitishwa kwa mdomo na ofisi ya Binjamin Netanyahu. Waziri wa Mambo ya Nje Eli Cohen amekaribisha uamuzi huu: "Hatua hii itaunganisha uhusiano kati ya Mataifa na watu".

Ilikuwa Desemba 2020, kama sehemu ya Makubaliano ya Abraham yaliyojadiliwa na Rais Donald Trump ambapo uhusiano kati ya Israeli na Morocco ulibadilika rasmi. Tangu wakati huo, ushirikiano katika nyanja za kijeshi, kiuchumi na utalii umeongezeka huku ukaribu huu ukiwatia wasiwasi raia. Kulingana na kura ya maoni iliyochapishwa mwaka wa 2022 na mtandao wa utafiti usioegemea upande wowote wa Arab Barometer, 31% raia wa Morocco wanaunga mkono kurejeshwa kwa uhusiano na Israel.

Ni nini hatimaye kiliwafanya Waisraeli waamue kuchukua hatua hii?

Mchakato wa maelewano kati ya Israel na Morocco ulianza mwaka wa 2020. Kwa hiyo itawachukua karibu miaka mitatu Wamorocco kupata kutoka kwa Waisraeli uungwaji mkono wanaotarajia kutoka kwa washirika wao wote: utambuzi kamili wa mamlaka yao kwa Sahara Magharibi, anakumbusha mwandishi mjini Jerusalem, Sami Boukhelifa.

Katika miaka ya hivi karibuni, Israel imezidisha ishara za nia njema kwa Morocco. Maafisa wakuu wa Israeli: mawaziri, maafisa wa jeshi walitembelea Morocco mara kwa mara, lakini kulibakia suala hili nyeti la mamlaka ya Morocco kwa Sahara Magharibi.

 Miezi michache iliyopita kumekuwa na hali ya utulivu kidogo katika uhusiano kati ya serikali ya Kiyahudi na ufalme wa Morocco. Rabat haikusita hivi karibuni kulaani ukoloni, ukandamizaji na unyanyasaji wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.