Pata taarifa kuu

Algiers yalaani hatua ya Israel ya kutambua mamlaka ya Morocco kwa Sahara Magharibi

Siku ya Jumatatu, Israel ilitambua rasmi mamlaka ya Morocco kwa eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi. Tangazo ambalo limeighadhabisha Algeria, ambayo inabaini kwamba uamuzi huu wa kidiplomasia ni "ukiukwaji wa wazi" wa sheria za kimataifa.

Sahara Magharibi na majirani zake.
Sahara Magharibi na majirani zake. RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa Algiers, Morocco na Israel wanatetea itikadi sawa, maono sawa ya ukoloni. Na uamuzi huu, uliochukuliwa na Israel na kutangazwa na baraza la mawaziri la kifalme huko Rabat, hivyo unaonyesha "maelewano ya sera za wavamizi, ushirikiano wao katika ukiukaji wa sheria za kimataifa".

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria inaendelea kwa kulaani "uvamizi wa haki halali ya watu wa Palestina ya kuanzisha nchi yao huru na Jerusalem kama mji mkuu wake na watu wa Saharawi kujitawala".

Wakati uhusiano wa nchi mbili kati ya Morocco na Algeria umevunjika tangu mwezi Agosti 2021, hatua hii inaonekana na serikali ya Algeria kama "kiungo kipya katika mfululizo vitendo na sera ya haraka iliyopitishwa na uvamizi wa Morocco".

Rabat inapanga kwa Sahara Magharibi, ambako mzozo wa eneo hili kubwa unahusisha tangu mwaka 1975 Morocco dhidi ya chama cha waasi wanaotaka kujitenga chama cha Polisario Front kinachoungwa mkono na Algeria, mpango wa kujitawala chini ya mamlaka yake ya kipekee. Polisario, kwa upande wake, ilitaka kuitishwe kura ya maoni ya kujitawala chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa, iliyopangwa wakati usitishaji mapigano ulipotiwa saini mwaka 1991, lakini haukufanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.