Pata taarifa kuu

Lualaba: Takriban watu 13 wakufa maji katika ajali ya boti kwenye Mto Kongo

Takriban watu 13 walifariki Jumanne, Novemba 21, katika ajali ya boti iliyozama kwenye Mto Kongo katika jimbo la Lualaba, ncini Hamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kulingana na Waziri wa Uchukuzi wa mkoa, Pitshou Nday, ambaye anathibitisha habari hii, ajali hii inlisababishwa na hitilafu za kiufundi na upakiaji kupita kiasi.

Meli iliyojaa kupita kiasi pamoja na boti tatu zinazopita kwenye Mto Kongo.
Meli iliyojaa kupita kiasi pamoja na boti tatu zinazopita kwenye Mto Kongo. Youtube
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo ilitokea usiku wakati boti hilo lilikuwa na abiria wengi na mizigo.

Abiria waliokuwa katika boti hilo walikuwa wanatoka katika eneo la uchimbaji madini ambapo kunachimbwa shaba na walikuwa wakienda katika kijiji cha Manfwe katika eneo la Mutshatsha, kama kilomita ishirini kutoka Kolwezi.

Kwa mujibu wa Pitshou Nday, baada ya kufika kilomita kadhaa kutoka kijiji hiki kutokana na hitilafu ya kiufundi na kuzidiwa wingi wa watu, jahazi hilo liligongana na kitu kilichokuwa ndani ya maji na kupinduka.

watu 13 wakiwemo wanaume 9, wanawake 3 na mtoto mchanga walifariki.

Pia kulikuwa na watu 5 walionusurika na bidhaa zote zilidondoka majini.

Pitshou Nday anasikitishwa kwamba wamiliki wa boti hawaheshimu hatua zilizochukuliwa hapo awali, kukataza safari za usiku kwenye Mto Kongo.

Aidha, anasikitishwa, majahazi mengi yanayofanya kazi usiku mara nyingi husafirisha bidhaa zaidi ya uwezo wao kinyume na inavyopendekezwa.

Ikiwa hatua hizi zote zingezingatiwa, ajali kama hizo hazingetokea, amesema Waziri wa Uchukuzi wa mkoa wa Lualaba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.