Pata taarifa kuu
USALAMA-BARABARANI

Kinshasa: Watu 5 wafariki katika mlipuko wa lori Righini

Watu watano wamefariki katika mlipuko wa lori lililokuwa limebeba mafuta Jumanne, Agosti 8, kwenye barabara ya By-pass katika wilaya ya Righini, wilaya ya Lemba (Kinshasa).

Mnamo 2010, mlipuko wa lori uliua zaidi ya watu 230 na kujeruhi karibu watu 100 nchini DRC.
Mnamo 2010, mlipuko wa lori uliua zaidi ya watu 230 na kujeruhi karibu watu 100 nchini DRC. RFI / Sébastien Nemeth
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii inatoka kwa meya wa manispaa ya Lemba na kuthibitishwa na makamu wa gavana wa Kinshasa, Gérard Mulumba na Waziri wa Mambo ya Ndani.

Aidha amebaini kuwa moto huo uliosambazwa na mlipuko wa lori hilo ulisababisha majeruhi 7 na uharibifu mwingine wa mali ikiwemo kuteketea kwa maduka kadhaa, duka kubwa na duka la vifaa vya ujenzi karibu na eneo la mkasa huu.

Vyanzo hivyovinaripoti kwamba lori hilo, lililokuwa likitokea katika mkoa wa Kongo-Central, iligonga nguzo ya nyaya za umeme za SNEL kabla ya kulipuka.

"Nilikuta lori la mafuta likiwaka moto. Kulingana na wenyeji wa wilaya hii, lori hili liligonga waya za umeme karibu na barabara ya Parc Virunga ambayo kwa kawaida huitwa Entrée du camp. Hivi ndivyo lori hili lililipuka na moto huu ulifuata njia za umeme, na kuteketeza maduka yote yaliyo kando ya Barabara ya By-Pass, "amesema shahidi mmoja akinukuliwa na Radio Okapi.

Kulingana na shahidi huyu, ajali hii iliyotokea mwendo wa saa nne asubuhi saa za Kinshasa, inafufua mjadala kuhusu tatizo la usafiri na usimamizi wa bidhaa zinazoweza kuwaka moto nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.