Pata taarifa kuu
USALAMA-BAHARINI

DRC: Takriban watu 100 wafariki baada ya boti kuzama Basankusu

Takriban abiria 100 wamekufa maji baada ya boti walizokuemo kuzama kwenye Mto Lulonga unaopatikana huko Basankusu, katika mkoa wa Equateur. Boti hizo zilikuwa zikielekea Lilanga, Congo-Brazzaville usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano Januari 18, mashahidi wanaripoti.

Mji wa Gbadolite, katika Mkoa wa Equateur, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mji wa Gbadolite, katika Mkoa wa Equateur, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Radio Okapi/John Bompengo
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Radio Okapi, inayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa nchini DRC, ikinukuu baadhi ya manusura siku ya Alhamisi Januari 19, walionusurika wanadai kupoteza bidhaa zote zikiwemo bidhaa za chakula na wanyama.

Hakuna operesheni ya uokoaji iliyofanyika hadi sasa kutafuta miili na watu waliotoweka, imebaini Radio Okapi ikinukuu Jean-Pierre Wangela, mkuu wa shirika la kiraia huko Basankusu.

“Kuna msafara wa boti unaoelekea Lilanga kila wakati. Boti hizo zilikuwa zimebeba watu wengi na bidhaa zao. Karibu usiku wa manane ajali hii ya boti ilitokea, na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha, zaidi au chini ya watu mia mbili. Lakini ikiwa wengine wameonusurika, ni kama watu hamsini na watano. Kulikuwa na hasara ya pesa na uharibifu wa wanyama. Hili lilitia hofu sana jiji la Basankusu,” anasema Jean-Pierre Wangela.

Inakadiriwa kuwa "karibu watu 145 hadi 150 walikufa maji". Jean-Pierre Wangela anafikiri kwamba upakiaji kupita kiasi ndio sababu kuu ya kuzama kwa meli hizi:

“Sababu ni kuzidiwa, kwa vile watu wamezoea, ni kwamba kwa sasa hakuna vyombo vya usafiri katika jimbo letu na hapa katika eneo la Basankusu. Kulikuwa na uzembe fulani kwa upande wa mwenye meli. Kwa kuwa bado ilikuwa ni lazima kuchota maji. Maji yaliingia hadi saa sita usiku, hivyo ndivyo mtumbwi ulivyozama”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.