Pata taarifa kuu
EAC- DRC- USALAMA

EAC yawataka raia wa DRC kuwa watulivu juhudi za kuleta amani zikiendelea

Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki EAC Dokta Peter Mathuki amewataka wananchi wa DRC kuwa watulivu wakati huu juhudi za kikanda na za kimataifa zinapoendelea kuhakikisha eneo hilo linakuwa salama. 

Nembo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Nembo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki http://eac.int/
Matangazo ya kibiashara

Dokta Mathuki ameitoa kauli hii wakati wa mkutano ulioandaliwa na tume ya Umoja wa Afrika pamoja na Jumuiya za Kiuchumi za kikanda kuhusu namna kukabiliana na Changamoto za kiusalama, kibiashara na mabadiliko ya tabia nchi.

“Kazi inaendelea kufanyika, tumejitolea kama EAC amani iwe DRC na tunaomba wanachi wote wawe na utulivu.”ameeleza Peter Mathuki.

Katika hatua nyingine Mkuu wa tume ya umoja wa Afrika, AU, Mousa Faki Mahamat amesema bara la Afrika sasa limepiga hatua katika kuwa na mikakati ya kuinua uchumi uliodorora kufuatia janga la Uviko 19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.