Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

DRC: UN inashirikiana na serikali kuchunguza mauaji ya halaiki Ituri

Ofisi ya umoja wa Mataifa nchini DRC, imesema inashirikiana na mamlaka za nchi hiyo, kufanya uchunguzi kuhusu maiti 50 zilizopatikana kwenye kaburi la pamoja mashariki mwa nchi hiyo ambako kunashuhudiwa utepetevu wa usalama.Mwanahabari wetu Emmanuel Makundi, anataarifa zaidi…

Kikosi cha askari wa Umoja wa Mataifa DRC, Monusco, wakipiga doria katika mitaa ya mkoa wa Ituru.
Kikosi cha askari wa Umoja wa Mataifa DRC, Monusco, wakipiga doria katika mitaa ya mkoa wa Ituru. SAMIR TOUNSI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tume ya walinda amani wa umoja wa Mataifa MONUSCO, wanajeshi wake walibaini kaburi hilo wakati wakifanya doria kwenye jimbo la Ituri, baada ya kupokea taarifa za mashambulio ya waasi wa CODECO juma lililopita.

Naibu msemaji wa umoja wa Mataifa, Farhan Haq, amesema miili ya watu 42, wakiwemo wanawake 12 na watoto 6 ilipatikana katika kijiji cha Nyamamba na Mbogi, ambapo wanachunguza ikiwa mauaji ya wiki iliyopita ya kundi la CODECO yanauhusiano na uvumbuzi wamakaburi haya.

Eneo la Ituri linalopakana na Uganda, siku za hivi karibuni linashuhudia hali tete ya usalama, kutokana na mashambulio ya mara kwa mara kati ya kundi la Codeco linalodai kuwakilisha jamii ya watu wa Lendu na lile la Zaire linalowakilisha jamii ya Hema.

Umoja wa amtaifa unasema watu zaidi ya 195 wameshauawa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, huku zaidi ya 84 wakitekwa nyara na ama upande mmoja wa makundi haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.