Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Upinzani wa Madagascar 'hautatambua matokeo' ya uchaguzi wa rais

Upinzani nchini Madagascar, ambao kwa kiasi kikubwa umewekwa ndani ya kundi moja, umetangaza Ijumaa jioni kwamba "hautatambua matokeo" ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais, ambayo itatangazwa siku ya Jumamosi.

Wanachama wa muungano wa upinzani waandamana katika mitaa ya wilaya ya Analamahitsy kupinga kufanyika kwa Uchaguzi wa urais wa mwaka 2023, huko Antananarivo, tarehe 14 Novemba 2023.
Wanachama wa muungano wa upinzani waandamana katika mitaa ya wilaya ya Analamahitsy kupinga kufanyika kwa Uchaguzi wa urais wa mwaka 2023, huko Antananarivo, tarehe 14 Novemba 2023. © AFP - RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

"Hatutatambua matokeo ya uchaguzi huu haramu, uliojawa na dosari, na tunakataa kuwajibika kwa msukosuko wa kisiasa na kijamii unaoweza kutokea," unaonya muungano wa wagombea kumi na mmoja wa upinzani katika taarifa, wakati kumi kati yao walitoa wito wa kususia uchaguzi wa Novemba 16.

Siteny Randrianasoloniaiko, ambaye alijitofautisha na kundi kwa muda kuongoza kampeni lakini ambaye alitia saini taarifa hiyo, pia alishutumu "machafuko yanayotia wasiwasi" ambayo "yalizua maswali halali kuhusu uhalali wa matokeo", amesema.

Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) inatazamiwa kutangaza matokeo shirikishi ya awali ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais Jumamosi asubuhi. Siku ya Ijumaa jioni, tovuti yake imeonyesha zaidi ya 91% ya kura zilizohesabiwa: rais anayemaliza muda wake Andry Rajoelina bado alikuwa akiongoza kwa kiasi kikubwa kwa 59.52 ya kura hizi, na kumwezesha kufikiria kushinda uchaguzi katika duru ya kwanza.

Andry Rajoelina ambaye alichaguliwa tangu 2018, aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mnamo 2009 kutokana na uasi uliomfukuza rais wa zamani Marc Ravalomanana.

Kulingana na makadirio kutoka kwa CENI, baadhi ya 60% ya waliojiandikisha hawakupiga kura mnamo Novemba 16. Wapiga kura milioni kumi na moja walipaswa kuchagua kati ya Bw. Rajoelina, 49, na wagombea wengine kumi na wawili. Lakini wagombea kumi wa upinzani, wakiwemo marais wawili wa zamani, walitoa wito kwa wapiga kura "kuzingatia kwamba chaguzi hizi hazipo". Walikataa kufanya kampeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.