Uchaguzi wa urais unafanyika nchini Madagascar
Nairobi – Raia wa Madagascar leo hii wanashiriki uchaguzi wa urais ambao umesusiwa na wagombea wengi wa upinzani huku kukiwa na hali ya wasiwasi nchini humo.
Imechapishwa:
Cheza - 00:54
Rais Andry Rajoelina ni miongoni mwa wagombea 13 wanaowania kiti cha urais huku wagombea 10 wa upinzani wakiwa wamekataa kushiriki na baadala yake kuwataka raia kususia zoezi hilo ,wakidai kumekuwa na mikakati ya kupendelea utawala uliopo madarakani.
Tangu oktoba mwaka huu, viongozi wa upinzani wakiwemo marais wawili wa zamani, wamekuwa wakifanya maandamano kupinga kila walichodai ni kutokuwepo kwa suala la uhuru na uwazi katika mikakati ya kuandaa uchaguzi huo.
Hapo jana polisi waliweka kafyu katika mji wa Antananarivo wakidai njama ya kuvuruga uchaguzi huo.
Rais Rajoelina aliingia madarakani mwaka 2009 baada ya mapinduzi ila hakuwania muhula uliofuata na akarejea madarakani mwaka 2018 na ameeleza matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi huu.