Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Madagascar: Sheria ya kutotoka nje yatangazwa Antananarivo kabla ya uchaguzi wa urais

Madagascar iimetangaza sheria ya kutotoka nje siku ya Jumatano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Antananarivo, inayotumika usiku mmoja kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais, ambao utafanyika katika mazingira ya wasiwasi baada ya wito wa kuususia kutoka kwa viongozi wakuu wa upinzani.

"Kutokana na vitendo mbalimbali vya hujuma vilivyotokea" Jumanne jioni, "nitatoa uamuzi hivi karibuni wa kutaganzwa sheria ya kutotoka nje kutoka saa 9:00 usiku hadi saa 4:00 usiku (Alfajiri)," gavana wa mji mkuu, Jenerali Angelo Ravelonarivo ametangaza wakati wa mkutano na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuchapishwa kwa nakala hiyo.
"Kutokana na vitendo mbalimbali vya hujuma vilivyotokea" Jumanne jioni, "nitatoa uamuzi hivi karibuni wa kutaganzwa sheria ya kutotoka nje kutoka saa 9:00 usiku hadi saa 4:00 usiku (Alfajiri)," gavana wa mji mkuu, Jenerali Angelo Ravelonarivo ametangaza wakati wa mkutano na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuchapishwa kwa nakala hiyo. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura milioni 11 waliojiandikisha wanaitwa kupiga kura siku ya Alhamisi kumchagua rais wao mpya. Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 6 asubuhi saa za Madagascar. Baada ya mwezi mmoja na nusu wa maandamano katika mitaa ya Antananarivo kwa wito wa upinzani, gavana wa mji mkuu, Jenerali Angelo Ravelonarivo, ameshutumu "vitendo vya hujuma" siku ya Jumatano.

"Kutokana na vitendo mbalimbali vya hujuma vilivyotokea" Jumanne jioni, "nitatoa uamuzi hivi karibuni wa kutaganzwa sheria ya kutotoka nje kutoka saa 9:00 usiku hadi saa 4:00 usiku (Alfajiri)," ametangaza wakati wa mkutano na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuchapishwa kwa nakala hiyo. Akirejelea "kuchomwa kwa kituo cha kupigia kura" na "kuharibiwa kwa vifaa mbalimbali vya uchaguzi", gavana huyo ameonya dhidi ya vitendo vinavyoweza kusababisha watu kukamatwa "katika kipindi hiki cha uchaguzi".

Wagombea 13 wanawania kiti cha urais, akiwemo rais anayemaliza muda wake Andry Rajoelina, mwenye umri wa miaka 49. Wagombea kumi wa upinzani walikusanyika kwa pamoja, wakiwemo marais wa zamani Hery Rajaonarimampianina na Marc Ravalomanana, waliwataka wapiga kura siku ya Jumanne kutopiga kura.

"Tunakataa uchaguzi wa Alhamisi na tunatoa wito kwa watu wote wa Madascar kuzingatia kuwa uchaguzi huu haupo," alitangaza mgombea na mpinzani Hajo Andrianinarivelo, 56, kwa niaba ya wagombea urais kumi. "Tunatoa wito kwa kila mtu kutopiga kura," aliongeza mgombea mwingine, Roland Ratsiraka, 57, akishutumu "udanganyifu".

Awamu ya kwanza ya maamuzi

Wanachama wa chama hicho walikataa kufanya kampeni huku mgombea wa serikali, ambaye anaweka dau la ushindi katika duru ya kwanza, katika wiki za hivi karibuni alikusanya maelfu ya wafuasi katika pembe nne za nchi ambako alikwenda kwa helikopta au kwa ndege ya kibinafsi.

Wapinzani wanapinga kustahiki kwa Rajoelina baada ya kashfa ya hivi majuzi kuhusu uraia wake wa nchi mbili na wanataka kusimamishwa kwa mchakato wa uchaguzi. Vyombo vya habari vilifichua mwezi Juni kwamba mkuu wa nchi anayeondoka alipata uraia wa Ufaransa mwaka 2014. Kulingana na upinzani, kwa hiyo alipoteza utaifa wake wa Madagascar na hawezi kuwa mgombea. Mahakama, hata hivyo, zilikataa rufaa hizo zikitaka kubatilisha ugombea wake.

Upinzani ulishutumu "mapinduzi ya kitaasisi" yenye lengo la kuhakikisha kuchaguliwa tena kwa Andry Rajoelina. Kudai uingiliaji kati kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, upinzani ulitangaza nia yake ya kuendeleza maandamano katika siku zijazo. Kufikia sasa, hata hivyo, maandamano yanayotawanywa mara kwa mara kwa mabomu ya machozi yamepata kuungwa mkono na washiriki mia chache tu.

Serikali ililaani "nia ya kupindua mamlaka", ikishutumu upinzani kwa "kutishia usalama wa nchi". Koloni hilo la zamani la Ufaransa, ambalo ni miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani, ambalo lilipata uhuruwake katika mwaka wa 1960 ni nadra sana kufanya uchaguzi bila ya mpito wa kijeshi au maandamano. Wapinzani pia wanashutumu hitilafu katika maandalizi ya uchaguzi, hasa kwenye orodha za wapiga kura. Wanataja kuwepo kwa "maelfu ya vituo vya kupigia kura vya uwongo".

Uchaguzi huo, uliyopangwa kufanyika Novemba 9, uliahirishwa kwa wiki moja mwezi uliopita kufuatia kuumia kwa mgombea wakati wa maandamano. Marekani na Umoja wa Ulaya walionyesha "wasiwasi" wao na kushutumu matumizi mabaya ya nguvu dhidi ya upinzani. Andry Rajoelina aliyechaguliwa mwaka wa 2018, aliingia mamlakani mwaka wa 2009 kutokana na uasi uliomwondoa madarakani Marc Ravalomanana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.