Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Madagascar: Mgogoro wazidi kutokota siku moja kabla ya uchaguzi wa rais

Mzozo wa kisiasa nchini Madagascar unazidi kuwa mbaya zaidi, siku moja kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, huku muungano ambao unawaleta pamoja wagombea kumi wa upinzani kwa kauli moja umetoa wito kwa wananchi wa Madagascar kutopiga kura.

Tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba, maandamano ya amani yaliyoitishwa namuungano unaowaleta pamoja wagombea kumi wa upinzani yameongezeka.
Tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba, maandamano ya amani yaliyoitishwa namuungano unaowaleta pamoja wagombea kumi wa upinzani yameongezeka. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tunakataa uchaguzi wa Alhamisi na tunatoa wito kwa watu wote wa Madagascar kuzingatia kwamba hakuna uchaguzi utakaofanyika," mgombea na mpinzani Hajo Andrianainarivelo, 56, ametangaza Jumanne jioni kwa niaba ya wagombea kumi wa upinzani kwa vyombo vya habari katika mji mkuu wa Antananarivo. "Tunatoa wito kwa kila mtu kutopiga kura," amesisitiza mpinzani na mgombea urais Roland Ratsiraka, 57, akishtumu "udanganyifu".

Tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba, maandamano ya amani yaliyoitishwa na muunganowa vyama vya upinzani yameongezeka. Na mvutano umeongezeka hivi karibuni. Wakiwa wametawanywa mara kwa mara kwa gesi ya kutoa machozi, waandamanaji walijibu Jumamosi kwa vifaa vya kujitengenezea nyumbani, wamebaini waandishi wa habari wa AFP. Watu kadhaa wamejeruhiwa katika wiki za hivi karibuni na wapinzani wamekamatwa kwa muda mfupi.

"Siku zote tumekuwa chini ya ukandamizaji, kupitia matumizi ya mabomu ya machozi," ameshutumu rais wa zamani wa Madagascar na mwanachama wa muungano wa upinzani, Hery Rajaonarimampianina, mwenye umri wa miaka 65. "Tunataka uchaguzi," ameeleza Bw. Andrianainarivelo lakini "tutaendelea na maandamano hadi kuwe na uchaguzi utakaokubaliwa na wote."

Wagombea 13 wako kwenye kinyang'anyiro hicho, akiwemo rais anayemalza muda wake Andry Rajoelina, mwenye umri wa miaka 49. Wanachama hao kumi walikataa kufanya kampeni huku mgombea wa serikali, ambaye anasema anategemea ushindi katika duru ya kwanza, katika wiki za hivi karibuni amekusanya maelfu ya wafuasi katika pembe nne za nchi ambapo alisafiri kwa helikopta au kwa ndege binafsi.

Hofu ya kutokuwa na utulivu

Serikali ya Rajoelina mara kwa mara imelaani "nia ya kupindua madaraka", ikishutumu upinzani kwa "kutishia kuhatarisha usalama wa nchi". Hofu ya kipindi kipya cha mpito kuitumbukiza nchi katika machafuko iko kwenye midomo ya kila mtu, katika kambi moja au nyingine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.