Pata taarifa kuu

Raia nchini Madagascar kushiriki uchaguzi mkuu wiki hii

Nairobi – Raia nchini Madagascar, Alhamisi ya wiki hii watapiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, baada ya majuma kadhaa ya upinzani kulalamika wakishinikiza uchaguzi huru na haki.

Uchaguzi wa  Madagascar
Rais anayeondoka madarakani Andry Rajoelina wakati akihotubia wapiga kura nchiniu Madagascar kuelekea uchaguzi mkuu REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Rais wa sasa, Andry Rajoelina, atachuana na wagombea wengine 12 wanaowania kuchaguliwa kuongoza kisiwa hicho kilichoko katika bahari ya hindi na mara nyingi kimeshuhudia vurugu wakati wa uchaguzi.

Kama ilivyokuwa katika uchaguzi uliopita, mwaka huu hakuna tofauti kwani tayari kumeshuhudiwa mgawanyiko mkubwa kisiasa kuanzia katika mahakama hadi kwenye mikutano ya kisiasa.

Uchaguzi nchini Madagascar
Polisi wamekuwa wakikabiliana na wafuasi wa upinzani kuelekea uchaguzi huo wa urais REUTERS - STRINGER

Mwezi Juni mwaka huu vyombo vya habari vilivripoti kuwa mwaka 2014 rais Rajoelina alichukua uraia wa Ufaransa, tarifa ambazo zilizidisha shinikizo kwa kiongozi huyo kujiuzulu.

Uchaguzi wa alhamisi unaenda kufanyika wakati ambapo kipindi cha kampeni kilitawaliwa na vurugu, ikiwemo polisi kutumia nguvu kubwa kukabiliana na wafuasi wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.