Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Mahakama ya Madagascar yaahirisha uchaguzi wa rais kwa wiki moja

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini Madagascar, uliopangwa kufanyika Novemba 9, imeahirishwa kwa wiki moja kufuatia kuumia kwa mgombea wakati wa maandamano ya upinzani, Mahakama Kuu ya Katiba imetangaza Alhamisi.

Mnamo Oktoba 2, mgombea Andry Raobelina alijeruhiwa usoni na kipande cha bomu la kutoa machozi huko Antananarivo. Kwa sasa anatibiwa nchini Mauritius.
Mnamo Oktoba 2, mgombea Andry Raobelina alijeruhiwa usoni na kipande cha bomu la kutoa machozi huko Antananarivo. Kwa sasa anatibiwa nchini Mauritius. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mahakama Kuu ya Katiba, kwa mujibu wa mamlaka yake ya udhibiti, inaamuru kuahirishwa kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais hadi Novemba 16, 2023," imsema mahakama ya juu zaidi ya Madagascar, nchi inayopatikana kwenye Bahari ya Hindi, katika uamuzi uliochapishwa kwenye tovuti yake. Duru ya pili ya uchaguzi wa urais itawekwa tarehe 20 Disemba lakini kampeni ya uchaguzi iliyoanza rasmi Jumatatu, inaongezwa kwa wiki moja.

Uchaguzi huo ambao rais anayemaliza muda wake Andry Rajoelina ni mgombea, umekuwa unaandaliwa kwa wiki kadhaa katika hali inayoendelea kuwa mbaya. Upinzani unashutumu njama ya wale walio mamlakani kumpendelea Rajoelina. Umoja wa Ulaya na Marekani zilisema mwezi uliopita walikuwa wakifuatilia maandalizi ya uchaguzi huo kwa "umakini mkubwa". Kwa jumla, wagombea kumi na watatu watashiriki kinyang'anyiro hiki cha urais.

Wengi wa wale ambao wanampinga Bw. Rajoelina katika uchaguzi huo, waliokusanyika katika muungano unaoitwa "collective of eleven", wametoa mwito wa maandamano karibu kila siku tangu mwanzoni mwa mwezi. Lakini mikusanyiko hii ilizuiwa na polisi kwa kutumia mabomu ya machozi.

Mnamo Oktoba 2, mgombea Andry Raobelina alijeruhiwa usoni na kipande cha bomu la kutoa machozi katikati mwa mji mkuu Antananarivo. Kwa sasa anatibiwa katika kisiwa jirani cha Mauritius.

Alikuwa amewasilisha ombi la kuahirishwa kwa uchaguzi kutokana na "dharura" iliyotokea. Mahakama ilikataa ombi lake, ikigundua kuwa Bw. Raobelina "amejiweka wazi hatarini kwa makusudi" kwa sababu "hatari ya kuumia wakati wa operesheni ya kuwatawanya waandamanaji na maafisa wa polisi ilikuwa inaonekana".

Mahakama kuu, hata hivyo, iliangazia "uhuru, uaminifu wa kupiga kura na usawa wa fursa kwa wagombea" kama masharti yasiyo na yasiyobadilika kwa uchaguzi "wa haki, uwazi na wa amani".

Andry Rajoelina, 49, aliingia madarakani mwaka 2009 kufuatia maasi yaliyomtimua Marc Ravalomanana. Kwa shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, aliacha kugombea mwaka 2013 lakini akachaguliwa mwaka 2018.

Mwezi uliopita, wagombea kumi wa upinzani walishutumu "mapinduzi ya kitaasisi" yaliyoratibiwa na wale waliokuwa madarakani: Mahakama Kuu ya Kikatiba ilikuwa imekataa rufaa tatu za kutaka kubatilishwa kwa ugombea wa Rajoelina "kwa kukosa uraia wa Madagascar". Mwishoni mwa mwezi Juni, habari za vyombo vya habari zilifichua kwamba ni raia wa Ufaransa aliyepewa uraia wa Madagascar mnamo 2014.

Mahakama ya juu zaidi nchini humo pia imeteua serikali ya muda inayoongozwa na Waziri Mkuu Christian Ntsay, rafiki wa karibu wa Rajoelina. Kwa mujibu wa Katiba wakati wa kipindi cha uchaguzi, rais aliacha kutumia mamlaka mwezi mmoja kabla ya uchaguzi.

Muda huo kwa kawaida ulipaswa kutekelezwa na rais wa Seneti, ambaye hata hivyo alikataa kwa "sababu za kibinafsi". Alitangaza wiki hii kuwa anabadili uamuzi wake na kwamba alikuwa chini ya "shinikizo" la kujiondoa. Siku ya Alhamisi, maseneta walikusanyika katika kikao kisicho cha kawaida kilichopigiwa kura na wengi kumtimua kwenye wadhifa wake kama rais wa Seneti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.