Pata taarifa kuu

Madagascar: Kumi na mbili wafariki katika mkanyagano katika uwanja wa michezo

Takriban watu kumi na wawili wamefariki siku ya  Ijumaa Agosti 25 nchini Madagascar katika mkanyagano kwenye mlango wa uwanja wa michezo katika mji mkuu, ametangaza Waziri Mkuu wa Madagascar, kisiwa kikubwa katika Bahari ya Hindi, Christian Ntsay. "Ripoti ya muda inataja watu kumi na wawili waliofariki" na wengine 80 waliojeruhiwa, amewaambia waandishi wa habari mbele ya hospitali ya Antananarivo, ambapo majeruhi wameelekwa.

Muonekano wa angani wa mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo.
Muonekano wa angani wa mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo. AFP - RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Mkanyagano huo ulitokea kwenye lango la kuingilia uwanja wa michezo wa Barea mjini Antananarivo, ambapo umati wa watazamaji wapatao 50,000 walifika kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Michezo ya kumi na moja ya visiwa vya Bahari ya Hindi.

Watu watakiwa kunyamaza kimya kwa muda wa dakika moja

Asili ya mkanyagano huo haijajulikana kwa sasa. Rais Andry Rajoelina, aliyekuwepo kwenye sherehe za michezo, ametoa wito wa watu kunyamanza kimya kwa muda wa dakika moja.

"Tulikuwa karibu 50,000 uwanjani," mkuu wa nchi amesema katika hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni. Lakini "tukio la kusikitisha lilitokea kwa sababu kulikuwa na mivutano. Kulikuwa na majeruhi na vifo mlangoni”. Huduma za dharura, polisi na jeshi wako eneo la tukio mpaka sasa, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP. Michezo ya Visiwa vya Bahari ya Hindi ni mashindano ya fani mbalimbali yanayofanyika mwaka huu nchini Madagascar hadi Septemba 3. Imekuwa ikifanyika kila baada ya miaka minne katika visiwa tofauti kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi kwa takriban miaka arobaini. Toleo la awali lilifanyika Mauritius.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.