Pata taarifa kuu

Transparency International yalalamikia matumizi mabaya ya misaada ya kibinadamu Madagascar

Shirika la kimataifa la Transparency International linasikitishwa na matumizi mabaya ya misaada ya kibinadamu iliyotumwa kwa wakazi wa maeneo ya kusini mwa Madagascar. Shirika hili limefanya mkutano hivi punde Jumatano mkutano na waandishi wa habari huko Antananarivo na kughadhabishwa na hali hiyo.

Watu wa Madagascar wanashiriki katika mpango wa usambazaji wa chakula wa WFP kusini mwa Madagascar.
Watu wa Madagascar wanashiriki katika mpango wa usambazaji wa chakula wa WFP kusini mwa Madagascar. AFP - RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Antananarivo, Laetitia Bezain

zaidi ya wakazi milioni 1.5 ambao wanakumbwa na ukame kwa miaka kadhaa, wako katika hali ya uhaba wa chakula katika sehemu hii ya kisiwa hicho. Kitengo cha Malina cha uchunguzi cha Transparency International, kimeangazia kupitia ushuhuda kutoka kwa wanavijiji na mamlaka za ndani vitendo vya rushwa na ubaguzi katika uteuzi wa walengwa wa misaada ya dharura. Utafiti huo, unaotangazwa kwenye kito cha Youtube cha Transparency International, unaangazia wilaya ya Ambovombe, mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukame na njaa.

Mifuko ya mchele, kunde, makopo ya mafuta lakini pia msaada wa kifedha wakati mwingine umeelekezwa kutoka kwa kaya zilizo hatarini zaidi, limebaini shirika la kimataifa la Transparency International. Shirika hili lisilo la kiserikali lilichunguza kuanzia mwezi Septemba 2022 hadi mwezi Machi 2023 msaada kutoka kwa shirika la Mpango wa Chakula Duniani na Mfuko wa Msdaada kwa Maendeleo, anasema Mialisa Randriamampianina, mhariri mkuu wa mtandao wa Malina:

“Wizi huo unafanyiwa kwa njia tofauti. Kwa mfano, tunao watu ambao wafanyakazi, wanaohamisha magunia ya mchele, wanachukua baadhi ya magunia na kuyapeleka mahal pengine. Pia tuna mamlaka zinazotoa vitambulisho vya uongo ili watu waweze kupata misaada ya kibinadamu. Ni mlolongo mzima wa makundi madogo madogo ya watu ambao hupeleka bidhaa kabisa kwa watu wengine na tunaishia na magunia ya mchele ambayo yanauzwa sokoni wakati kawaida ni magunia ya mchele ambayo yalipaswa kusambazwa kwa watu. (…) Uchunguzi huu unaweza kusaidia mamlaka na taasisi zinazosimamia msaada huu kutafakari jinsi ya kuboresha usimamizi wake kwa sababu ni maisha ya watu ambayo yako hatarini.”

"Katika misaada ya kifedha, mashahidi wetu pia wanashutumu ukweli kwamba wamepokonywa msaada huu mara tu wanapopokea kiasi hicho", anaelezea Ketakandriana Rafitoson, mkurugenzi mtendaji wa Mpango wa Kimataifa wa Transparency nchini Madagascar.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani nchini Madagascar limebaini kwamba liko katika mchakato wa kukagua taarifa hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.