Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Mfungwa kwa jaribio la mapinduzi nchini Madagascar ahamishiwa Ufaransa

Afisa wa zamani wa jeshi wa cheo cha kanali katika jeshi la Ufaransa, Philippe François, aliyehukumiwa na mahakama ya Madagascar miaka kumi ya kufanya "kazi za kijamii" kwa mapinduzi ya kijeshi na jaribio la kumuua Rais Rajoelina, amehamishiwa nchini Ufaransa siku ya Ijumaa, kulingana na vyanzo kadhaa vya kisiasa.

Nchini Madagascar, kazi za kijamii ilifutwa mwaka 2010 lakini dhana hiyo ilibaki na inalingana kiutendaji na kifungo jela.
Nchini Madagascar, kazi za kijamii ilifutwa mwaka 2010 lakini dhana hiyo ilibaki na inalingana kiutendaji na kifungo jela. © Laetitia Bezain/RFI
Matangazo ya kibiashara

"Amehamishwa leo (Ijumaa)," chanzo cha kisiasa cha Madagascar kimeliambia shirika la habari la AFP. "Ni kuhamishwa wala sio kumsafirisha kufungwa huko", kimeeleza chanzo kingine cha kisiasa, kikibaini kwamba uhamisho huu unamuwezesha mfungwa huyo wa Ufaransa kutumikia kifungo chake nchini Ufaransa, ambako alitakiwa kufika mchana kupitia kisiwa cha Réunion.

Bw. François, 55, alikamatwa nchini Madagascar mnamo mwezi Julai 2021 katika kesi inayoitwa "Apollo 21". Mahakama ya mwanzo ilimhukumu mwaka huo huo, uamuzi uliothibitisha mwaka uliofuata katika Mahakama ya Juu. Alifungwa tangu kukamatwa kwake katika gereza lenye ulinzi mkali la Tsiafahy, viungani mwa mji mkuu Antanarivo.

Nchini Madagascar, kazi za kijamii ilifutwa mwaka 2010 lakini dhana hiyo ilibaki na inalingana kiutendaji na kifungo jela. Jumla ya watu 20 wamehusishwa katika kesi hiyo, wakiwemo askari wa kikosi maalum wanaoshukiwa kuajiriwa kwa minajili ya kufanya mapinduzi wakati wa operesheni iliyopewa jina la "Apollo 21".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.