Pata taarifa kuu

Kimbunga Freddy chaelekea Msumbiji, watu 5 wafariki nchini Madagascar

Kimbunga cha kitropiki Freddy, ambacho kinafagia Bahari ya Hindi, kilikuwa njiani kikielekea Msumbiji Jumatano jioni, baada ya kupoteza nguvu lakini kusababisha vifo vya watu watano nchini Madagascar.

Wataalamu wa hali ya hewa wa Ufaransa wakifuatilia kimbunga Freddy kutoka kituo cha Saint-Denis de la Réunion, Februari 20, 2023.
Wataalamu wa hali ya hewa wa Ufaransa wakifuatilia kimbunga Freddy kutoka kituo cha Saint-Denis de la Réunion, Februari 20, 2023. AFP - RICHARD BOUHET
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya raia 16,600 wa Madagascar kwa jumla wameathirika, huku baadhi ya nyumba 4,500 zikikumbwa na mafuriko au kuharibiwa, imesema Ofisi ya Kitaifa ya Kudhibiti Hatari (BNGRC). Maelfu ya watu walikuwa wamewekwa katika makazi ya dharura kama hatua ya kuzuia athari zaidi. Kiwango kamili cha uharibifu kinatathminiwa.

Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Ufaransa imesema Kimbunga Freddy kimepunguza kasi kilipokuwa kipita Madagascar na kasi ya wastani ya upepo ilishuka hadi kilomita 55 kwa saa. Lakini mamlaka hiyo imeonya kuwa kimbunga hicho kitaendelea kupiga hatua kuelekea bara la Afrika. Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Ufaransa imeonya kwamba kinaweza kurejesha nguvu katika maji ya joto ya Mfereji wa Msumbiji.

Kimbunga freddy kinatarajiwa siku ya Ijumaa kupiga katika maeneo kati ya katikati na kusini mwa Msumbiji, zaidi ya kilomita 500 kaskazini mwa mji mkuu Maputo, na huenda kikafika Zimbabwe. Serikali ya Msumbiji imetoa tahadhari nyekundu na kuweka huduma za idara ya huduma ya dharura katika tahadhari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.