Pata taarifa kuu

Kimbunga Ana chasababisha vifo Madagascar, Msumbiji na Malawi

Kimbunga kilichopewa jina la Ana, kimewauwa watu 46 nchini Madagascar, Msumbiji na Malawi na kusababisha mafuriko makubwa.

Nchini Madagascar pekee, watu 39 walipoteza masiha na wengine zaidi ya 65,000 kuachwa bila makao kuanzia wiki iliyopita.
Nchini Madagascar pekee, watu 39 walipoteza masiha na wengine zaidi ya 65,000 kuachwa bila makao kuanzia wiki iliyopita. AFP - RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Kimbunga hicho kilianzia katika Kisiwa hicho kikubwa barani Afrika na kusababisha mvua kubwa, iliyosababisha mafuriko makubwa jijini Antananarivo.

Nchini Madagascar pekee, watu 39 walipoteza maisha na wengine zaidi ya 65,000 kuachwa bila makaazi kuanzia wiki iliyopita.

Nchini Msumbiji, watu watatu wamepoteza maisha, huku wengine zaidi ya 49 wakijeruhiwa katika mkoa wa Zambezia. Nchini Malawi, watu wanne wamepoteza maisha.

Watu wengine zaidi la Laki tano wameyahama makaazi yao kufuatia kimbunga hicho na kukimbilia katika mikoa ya Zambezia, Nampula na Sofala kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Msumbiji na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Watalaam wa utabiri wa hali ya hewa, nchini Msumbiji wanasema, huenda kukashuhudiwa kwa vimbunga vinne kati ya sita katika ukanda huo, mpaka mwezi Machi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.