Pata taarifa kuu
BURMA-JAMII

Watu wengi watoweka baada ya maporomoko ya udongo kwenye mgodi kaskazini mwa burma

Takriban watu 70 hawajulikani walipo na mmoja ameripotiwa kufariki dunia baada ya maporomoko ya udongo, tukio lililotokea Jumatano (Desemba 22) kaskazini mwa Burma, afisa wa idara za uokoaji ameliambia shirika la habari la AFP.

Wafanyakazi katika mgodi wa Hpakant katika Jimbo la Kachin, Burma.
Wafanyakazi katika mgodi wa Hpakant katika Jimbo la Kachin, Burma. © REUTERS/Soe Zeya Tun
Matangazo ya kibiashara

Gazeti la "Kachin News", kwa upande wake, limetangaza kwamba watoto ishirini wamepoteza maisha katika maporomoko haya ya udongo.

"Watu walio kati ya 70 na 100 wametoweka katika maporomoko ya udongo yaliyotokea mwendo wa saa nne asubuhi" katika mgodi wa Jade huko Hpakant, jimbo la Kachin, afisa wa idara ya za dharura Ko Ny ameliambia shirika la habari la AFP. "Tulipeleka majeruhi 25 hospitalini, huku tukigundua kuwa mmoja amefariki," ameongeza. Takriban maafisa 200 wa idara ya uokoaji wanashiriki katika operesheni hii kutafuata miili ya watu na watu ambao bado wanaaminika kuwa wako hai, wengine wakiwa kwenye boti kujaribu kuopoa miili kutoka ziwani, amebaini. Kulingana na idara ya Zima moto, maafisa wa idara hiyo kutoka Hpakant na mji jirani wa Lone Khin pia wanashiriki katika shughuli za uokoaji, lakini hawakuoa ripoti yoyote.

Nchini Burma, wachimbaji kadhaa hufa kila mwaka wakifanya kazi katika mazingira hatarishi katika machimbo ya Jade, tasnia isiyo wazi na isiyodhibitiwa vyema. Maporomoko ya udongo yanatokea mara kwa mara katika eneo hili duni na gumu kufikiwa, ambalo linaonekana kama eneo hatari kwani limebadilishwa na makundi makubwa ya wachimbaji madini, bila kujali mazingira.

Migodi ya siri

Kufuatia kusitishwa kwa shughuli ya uchimbaji madini mwaka 2016, migodi mingi mikubwa imefungwa na haifuatiliwa tena, na kuruhusu kurudi kwa wachimbaji wengi wa kujitegemea. Watu kutoka jamii za makabila duni, makabila haya yanafanya sughuli hii kwa kisiri katika maeneo yaliyoachwa na wachimbaji. Mvua kubwa zilisababisha maafa makubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo mwaka wa 2020, huku wachimba migodi 300 wakizikwa baada ya maporomoko ya udongo kutokea katika eneo la Hpakant, kitovu cha tasnia hii, karibu na mpaka wa China.

Burma inapata mapato makubwa kutokana na uwepo mkubwa katika udongo wake wa mawe ya thamani ambayo yanathaminiwa sana nchini China. Biashara ya Jade inazalisha zaidi ya dola bilioni 30 kwa mwaka, karibu nusu ya pato la taifa. Mapinduzi ya Februari yaliharibu nafasi ya kupata mageuzi ya sekta yaliyoanzishwa chini utawala wa Aung San Suu Kyi, shirika la Global Witness lilisema katika ripoti iliyotolewa mwaka wa 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.