Pata taarifa kuu
MYANMAR-USALAMA

UN yaonya kuwa Myanmar yaweza kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe

Maafisa wakuu wawili wa Umoja wa Mataifa walionya wiki hii kwamba Myanmar inaweza kutumbukiwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Operesheni ya vikosi vya usalama vya Myanmar katika kaunti ya Kamayut huko Yangon Machi 2021. Kwa upande wa wajumbe wa Umoja wa Mataifa wanasema, kurudi kwa demokrasia nchini Myanmar ni kama ndoto.
Operesheni ya vikosi vya usalama vya Myanmar katika kaunti ya Kamayut huko Yangon Machi 2021. Kwa upande wa wajumbe wa Umoja wa Mataifa wanasema, kurudi kwa demokrasia nchini Myanmar ni kama ndoto. AP
Matangazo ya kibiashara

Tangu mapinduzi ya kijeshi Februari 1, jeshi linaloshikilia madaraka, limeendelea kuongeza msako na ukandamizaji wa umwagaji damu kwa raia wa Myanmar.

Ikiwa maelfu ya watu waliachiliwa mapema wiki hii, zaidi ya wapinzani 100 walikamatwa tena. Kwa upande wa wajumbe wa Umoja wa Mataifa wanasema, kurudi kwa demokrasia nchini Myanmar ni kama ndoto.

Wapinzani dhidi ya utawala wa kijeshi wamekimbilia Kaskazini mwa nchi, lakini pia huko ndiko jeshi "linakusanya makumi ya maelfu ya wanajeshi na silaha nzito" kulingana na Tom Andrews, mwandishi wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nchini Myanmar , ambaye anasema ana hofu kuwa "vitendo vingi vya ukatili vitatendeka dhidi ya wakosoaji wa serikali".

Hofu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe

Tom Andrews sio wa kwanza wiki hii kupaza sauti dhidi ya hali hiyo nchini Myanmar: Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Myanmar, Christine Schraner Burgener, raia wa Uswisi, ameelezea hofu yake kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaweza kuzuka nchini humo.

Kulingana Christine Schraner Burgener, jeshi la myanmar hutumia mbinu kadhaa dhidi ya raia: kuchoma vijiji, visa vya uporaji vya mara kwa mara, kukamatwa kwa watu wengi lakini pia kuwatesa na kuwanyonga wafungwa.

 "Uhalifu unaowezekana dhidi ya binadamu"

Ukatili huu, ulioripotiwa kwa miezi kadhaa, unaungana na hitimisho la Tom Andrews: kwake anaona kuwa utawala wa kijeshi ncini Myanmar umeendeleza "uhalifu unaowezekana dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita".

Wajumbe wa Umoja wa Mataifa wamekumbusha kwamba "mbinu hizi ni kumbukumbu mbaya ya zile zilizotumiwa na vikosi vya jeshi kabla ya mashambulio yao ya mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya watu wachache ya Rohingya katika Jimbo la Rakhine mnamo mwaka 2016 na 2017".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.