Pata taarifa kuu
MYANMAR-HAKI

Burma: Utawala wa kijeshi wamnyamanzisha wakili Aung San Suu

Wakili mkuu wa Aung San Suu Kyi hana haki tena ya kuzungumza na vyombo vya habari, wanadiplomasia wa kigeni na mashirika ya kimataifa, wametangaza leo Ijumaa (Oktoba 15) kwenye mitandao ya kijamii.

Utawala wa jeshi uko madarakani tangu mapinduzi ya Februari 1 dhidi ya Aung San Suu Kyi (kwenye picha).
Utawala wa jeshi uko madarakani tangu mapinduzi ya Februari 1 dhidi ya Aung San Suu Kyi (kwenye picha). Sai Aung Main AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa jeshi, madarakani tangu mapinduzi ya Februari 1 dhidi ya Aung San Suu Kyi, ulitoa agizo hilo ambalo wakili huyo aliweka kwenye ukurasa wake wa Facebook, shirika la habari la AFP limebaini.

Ifahamu Burma au Myanmar

Zamani ikiitwa Burma, Myanmar ni nchi inayokutikana Mashariki mwa Asia yenye makundi zaidi ya 100 ya kikabila. Inapakana na India, Bangladesh, China, Laos na Thailand.

Mnammo mwaka 1989 serikali ya kijeshi ilizibadilisha rasmi tafsiri nyingi za majina mengi ya Kiingereza yaliotumika tangu enzi za ukoloni wa Burma, likiwemo jina la nchi lenyewe: "Burma" ikawa "Myanmar".

Ubadilishaji huo wa majina umeendelea kuzua mabishano ambapo makundi mengi ya upinzani wa kisiasa na kikabila pamoja na mataifa yanaendelea kutumia "Burma" kwa sababu hawatambui uhalali wa serikali ya kijeshi au mamlaka ya kubadili jina la nchi.

Mara baada ya kuchukuwa madaraka Aprili 2016, Aung San Suu Kyi alifafanua kuwa wageni wana uhuru wa kutumia jina lolote kati ya hayo mawili, "kwa sababu hakuna katika katiba yetu, panaposema kwana unalaazimika kutumia neno makhsusi kwa wakati fulani."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.