Pata taarifa kuu
BURMA-SIASA

Kesi ya Aung San Suu Kyi kuanza kusikilizwa Jumatatu Juni 14 Burma

Aung San Suu Kyi, kiongozi aliyechaguliwa kisha kutimulia mamlakani kwa mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1, anakabiliwa na mashtaka mengi, ikiwa ni pamoja na uchochezi pamoja na kuvunja sheria ya siri za serikali.. Kesi yake itaanza kusikiliwza Jumatatu Juni 14.

Aung San Suu Kyi, picha iliyopigwa mwaka 2016.
Aung San Suu Kyi, picha iliyopigwa mwaka 2016. AFP - YE AUNG THU
Matangazo ya kibiashara

Wakili wa Aung San Suu Kyi, Min Min Soe, amesema baada ya kukutana kwa mazungumzo katika mji mkuu wa Naypyidaw na kiongozi huyo wa zamani akiwa kizuizini nyumbani, kwamba ushuhuda utaanza kutolewa Jumatatu, Juni 14. "Ameomba kila mtu kuwa na afya njema," ameaongeza.

Akabiliwa na mashtaka mengi

Aung San Suu Kyi, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 1991, anakabiliwa na mashitaka sita tangu kukamatwa kwake, ikiwa ni pamoja na lile la kuchochea machafuko ya umma.

Tangu mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1, Aung San Suu Kyi mwenye umri wa miaka 75 ameweza tu kukutana na mawakili wake mara mbili.

Kiongozi huyo wa zamani alionekana hadharani Mei 24, kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake nyumbani, wakati alifikishwa mahakamani. Uongozi wa utawala wa kijeshi umetishia kuvunja chama chake cha kisiasa, National League for Democracy (LND), ambacho kilishinda kwa kura nyini uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2020, na baadae kushtumiwa udanganyifu wakati wa uchaguzi huu.

Raia 850 waliangamia katika makabiliano na jeshi

Karibu watu  850 waliuawa nchini Burma tangu Februari 1 katika maandamano yaliyokandamizwa na vikosi vya usalama na ulinzi , kulingana na shirika linalotoa msaada kwa Wafungwa wa Kisiasa (AAPP).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.