Pata taarifa kuu
MYANMAR

Suu Kyi kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu mapinduzi ya kijeshi

Kiongozi wa zamani wa kiraia wa Myanmar Aung San Suu Kyi ana afya njema na atafikishwa mahakamani hivi karibuni, amesema iongozi wa utawala wa kijeshi madarakani tangu mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1.

Wahamiaji wanaoandamana dhidi ya mamlaka ya kijeshi nchini Myanmar wanashikilia picha za kiongozi Aung San Suu Kyi, huko Bangkok, Thailand, Machi 28, 2021.
Wahamiaji wanaoandamana dhidi ya mamlaka ya kijeshi nchini Myanmar wanashikilia picha za kiongozi Aung San Suu Kyi, huko Bangkok, Thailand, Machi 28, 2021. REUTERS - JORGE SILVA
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Min Aung Hlaing alikuwa akiongea kwenye mahojiano ya runinga yaliyorekodiwa siku ya Alhamisi na kituo cha Televisheni cha Phoenix cha Hong Kong, ambacho hakijarusha mahojiano hayo lakini sehemu yake imerushwa kwenye mitandao ya kijamii leo Jumamosi.

"Aung San Suu Kyi anaendelea vizuri kiafya. Yuko nyumbani na atafikishwa mahakamani katika siku chache zijazo" , amesema jenerali katika video hiyo, akizungumza kwa lugha ya Kiburma na tafsiri kwa lugha ya Kichina iliyotolewa na kituo cha televisheni.

Viongozi wa kijeshi washindwa kusifu kazi aliyoifanya Suu Kyi

Alipoulizwa kuhusu rekodi ya kisiasa ya Bi Suu Kyi, almejibu: "kwa kifupi, alifanya kile alichoweza".

Bi Suu Kyi, 75, hajaonekana hadharani tangu kukamatwa kwake nyumbani huko Naypyidaw wakati wa mapinduzi ya kijeshi. Anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Jumatatu wiki ijayo.

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 1991 ameshtakiwa mara sita tangu kukamatwa kwake. Anashtakiwa hasa kwa kukosa kufuata masharti yanayohusiana na janga la Corona, uingizaji haramu wa raia wa kigeni, uchochezi wa machafuko na ukiukaji wa sheria za siri za serikali za tangu enzi za ukoloni.

Pia anatuhumiwa kukusanya dola laki kadhaa na kilo kumi na moja za dhahabu kwa hongo, lakini hajashtakiwa kwa "ufisadi"

Ikiwa atapatikana na hatia, anaweza kupigwa marufuku kujihusisha na siasa, hata akahukumiwa kifungo cha miaka mingi gerezani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.