Pata taarifa kuu
CHINA-USHIRIKIANO

Burma: China kufadhili miradi ya maendeleo kwa makubaliano na utawala wa kijeshi

China itatoa zaidi ya dola milioni sita kwa serikali ya Burma kufadhili miradi ya maendeleo nchini, Wizara ya Mambo ya Nje ya Burma imetangaza leo Jumatano.

Wapinzani wa utawala wa kijeshi wameshutumu China kwa kuunga mkono hatua ya jeshi kudhibiti madaraka ambapo Aung San Suu Kyi, kiongozi aliyechaguliwa, aliondolewa madarakani na kuwekwa chini ya ulinzi.
Wapinzani wa utawala wa kijeshi wameshutumu China kwa kuunga mkono hatua ya jeshi kudhibiti madaraka ambapo Aung San Suu Kyi, kiongozi aliyechaguliwa, aliondolewa madarakani na kuwekwa chini ya ulinzi. REUTERS - Stringer .
Matangazo ya kibiashara

Tofauti na nchi za Magharibi, ambazo zililaani hatua ya jeshi kushikilia madaraka Februari 1, China imetangaza kwamba vipaumbele vyake ilikuwa utulivu na nchi za kigeni kutoingilia masuala ya ndani ya jirani yake.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Burma imesema fedha zilizotumwa na China zitatumika katika sekta za utamaduni, kilimo, sayansi, utalii na kuzuia majanga ya asili.

Makubaliano yalitiwa saini Jumatatu wiki hii na balozi wa China nchini Burma, kulingana na taarifa Wizara ya Mambo ya Nje ya Burma. Ubalozi wa China ulithibitisha kutiwa saini kwa makubaliano hayo kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Wapinzani wa utawala wa kijeshi wameshutumu China kwa kuunga mkono hatu ya jeshi kudhibiti madaraka ambapo Aung San Suu Kyi, kiongozi aliyechaguliwa, aliondolewa madarakani na kuwekwa chini ya ulinzi. Beijing imemfutilia mbali shutma hizo na kusema inaunga mkono diplomasia ya kikanda katika mgogoro huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.