Pata taarifa kuu
BURMA-SIASA

Burma: Mwandishi wa habari wa Marekani akabiliwa na kifungo cha maisha

Viongozi wa kijeshi nchini Burma wameendelea kuonyesha nguvu zao na hawataki mtu kuingilia mambo yao. Mwandishi wa habari wa Marekani Danny Fenster yuko katika hali ngumu.

Kiongozi wa Burma Min Aung Hlaing.
Kiongozi wa Burma Min Aung Hlaing. AP
Matangazo ya kibiashara

Alikamatwa wakati akijaribu kuondoka nchini Burma mwezi Mei, anakabiliwa na "mashtaka mawili chini ya Ibara ya 50 (a) ya sheria ya kupambana na Ugaidi na Ibara ya 124 (a) ya sheria hiyo," wakili wake Than Zaw Aung ameliambia shirika la habari la AFP.

Hukumu chini ya sheria ya kupambana na ugaidi hutoa adhabu ya kifungo cha maisha jela. Danny Fenster mwenye umri wa miaka 37 alikuwa tayari anashitakiwa kwa kuchochea vurugu, kushiriki katika makundi haramu na kwa kuvunja sheria ya uhamiaji.

Mashtaka hayo mapya yanakuja siku chache baada ya mwanadiplomasia wa zamani wa Marekan na msuluhishi katika masuala ya mateka Bill Richardson kukutana na kiongozi wa kijeshi Min Aung Hlaing katika mji mkuu wa Naypyidaw. Wawili hao walijadili suala la utoaji wa chanjo ya Covid-19 na vifaa vya matibabu, kulingana na jeshi.

Kurejea kwa udikteta

Mwandishi huyo wa habari wa Marekani anasemekana kuwa aliambukizwa virusi vya Corona vinavyosababisha Covid-19 akiwa kizuizini, familia yake imesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa Marekani mwezi Agosti. Burma imekumbwa katika machafuko tangu mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1 ambayo yalisitisha miaka 10 ya demokrasia nchini humo.

Utawala unaendelea na msako mkali dhidi ya wapinzani, huku zaidi ya raia 1,200 wakiripotiwa kuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.