Pata taarifa kuu
BURMA-HAKI

Utawala wa kijeshi wamhukumu U Win Htein, kifungo cha miaka 20 jela

Utawala wa kijeshi nchini Burma umemhukumu mshirika wa karibu wa kiongozi wa kiraia aliyetimuliwa madarakani Aung San Suu Kyi kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la uhaini, wakili wake ametangaza.

Win Htein, kiongozi wa chama cha National League for Democracy (LND), pamoja na Waziri Mkuu Aung San Suu Kyi, waliokamatwa wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1, 2021.
Win Htein, kiongozi wa chama cha National League for Democracy (LND), pamoja na Waziri Mkuu Aung San Suu Kyi, waliokamatwa wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1, 2021. AFP
Matangazo ya kibiashara

"U Win Htein amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela chini ya kifungu cha 124a na mahakama maalum," mwanasheria wake Myint Thwin ameliambia shirika la habari la AFP, na kuongeza kuwa watakata rufaa.

Mbunge huyo wa zamani ni mwanachama wa kwanza wa ngazi ya juu wa National League for Democracy, chama cha Aung San Suu Kyi, kuhukumiwa na utawala wa kijeshi. Mzee huyo mwenye umri wa miaka 80 ni mfungwa wa kisiasa wa muda mrefu ambaye kwa muda mrefu amekuwa akifanya kampeni dhidi ya utawala wa kijeshi, akiwa kizuizini na baada ya kuachiliwa huru.

Mtu wa hadhi ya kimataifa

U Win Htein ambaye anachukuliwa kkama mshirika wa karibu wa Aung San Suu Kyi, mara nyingi amekuwa akiombwa na vyombo vya habari vya kimataifa - kama vile RFI - na vyombo vya habari vya nchini Burma ili kujua maoni ya mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 1991.

Kabla ya kukamatwa siku tatu baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1, aliviambia vyombo vya habari vya Burma kwamba mapinduzi hayo hayakuwa dhihirisho la hekima kubwa na kwamba wahalifu wake "wanaipeleka (nchi) katika mwelekeo mbaya".

Aung Suu Kyi anakabiliwa na mashtaka kadhaa ambayo yanaweza kumpeleka gerezani kwa miongo kadhaa, ikiwa ni pamoja na uingizaji haramu wa vifaa vya kuongea na kutofuata sheria za kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu. Alitoa ushahidi kwa mara ya kwanza katika mahakama ya kijeshi siku ya Jumanne, miezi minne baada ya kuhukumiwa na jeshi, chanzo kinachofahamu suala hilo kimeiambia AFP. Vyombo vya habari havikuruhusiwa kutazama kesi ya kiongozi huyo katika mahakama maalum ya Naypyidaw, mji mkuu uliojengwa na majenerali, na hivi majuzi utawala wa kijeshi ulipiga marufuku timu yake ya wanasheria kuzungumza na vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.