Pata taarifa kuu

Takriban watu 12 wafariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Afghanistan

Tetemeko la ardhi lilisababisha vifo vya watu 12 na wengine kasdhaa kujeruhiwa Jumatatu magharibi mwa Afghanistan, mamlaka nchini humo imesema. Tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa 5.6 kwenye vipimo vya Richter, kulingana na Taasisi ya Marekani inayohusika na matetemeko ya ardhi (USGS).

Waathiriwa wameangamia wakati nyumba zao katika wilaya ya Qadis, mkoa wa Badghis, zilipoporomoka, gavana wa wilaya Mohammad Saleh ameliambia shirika la habari la AFP.
"Pia kunaripotiwa majeruhi katika tetemeko hili la ardhi," afisa huyo wa Afghanistan amesema, akibaini kwamba wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa waathiriwa.
Afghanistan hukumbwa na matetemeko ya ardhi mara kwa mara, hasa katika eneo la milima ya Hindu Kush ambayo iko kwenye makutano ya miamba ya Eurasia na India. Matetemeko haya ya ardhi yanaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwa sababu ya ubovu wa majengo nchini Afghanistan.
Waathiriwa wameangamia wakati nyumba zao katika wilaya ya Qadis, mkoa wa Badghis, zilipoporomoka, gavana wa wilaya Mohammad Saleh ameliambia shirika la habari la AFP. "Pia kunaripotiwa majeruhi katika tetemeko hili la ardhi," afisa huyo wa Afghanistan amesema, akibaini kwamba wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa waathiriwa. Afghanistan hukumbwa na matetemeko ya ardhi mara kwa mara, hasa katika eneo la milima ya Hindu Kush ambayo iko kwenye makutano ya miamba ya Eurasia na India. Matetemeko haya ya ardhi yanaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwa sababu ya ubovu wa majengo nchini Afghanistan. AFP
Matangazo ya kibiashara

Waathiriwa wameangamia wakati nyumba zao katika wilaya ya Qadis, mkoa wa Badghis, zilipoporomoka, gavana wa wilaya Mohammad Saleh ameliambia shirika la habari la AFP.

"Pia kunaripotiwa majeruhi katika tetemeko hili la ardhi," afisa huyo wa Afghanistan amesema, akibaini kwamba wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa waathiriwa.

Afghanistan hukumbwa na matetemeko ya ardhi mara kwa mara, hasa katika eneo la milima ya Hindu Kush ambayo iko kwenye makutano ya miamba ya Eurasia na India. Matetemeko haya ya ardhi yanaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwa sababu ya ubovu wa majengo nchini Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.