Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa yahitaji zaidi ya dola bilioni tano kusaidia Afghanistan

Afghanistan ambayo inakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi inahitaji msaada wa haraka kukidhi mahotaj muhimu. Umoja wa Mataifa unaomba zaidi ya dola bilioni tano kusaidia Afghanistan mwaka wa 2022. Kiwango hicho cha fedha ni kikubwa zaidi kuwahi kuombwa kulisaidia taifa moja.

Afghanistan ina watu milioni 23 wanaohitaji msaada wa kibinadamu.
Afghanistan ina watu milioni 23 wanaohitaji msaada wa kibinadamu. AP - Petros Giannakouris
Matangazo ya kibiashara

Miezi sita baada ya Taliban kuchukua mamlaka, zaidi ya nusu ya watu wako kwenye hatari ya kukabiliwa na njaa kali. Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuepuka "janga" hili. Na kuahidi kwamba fedha zitakazotolewa hazitakabidhiwa utawala wa Taliban.

"Ikiwa nchi itasambaratika kabisa, basi tutaona mzozo mkubwa zaidi wa wahamiaji. Ni vigumu kuwa wazi zaidi kuliko amesema Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi. Afghanistan ina watu milioni 23 wanaohitaji msaada wa kibinadamu. Ikiwa ni pamoja na watu milioni tisa waliokimbia makazi yao, na watoto milioni moja ambao wanaweza kufa kwa njaa ikiwa hakuna msaada unaowafikia.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths anatoa wito kwa mataifa kutowapa kisogo Waafghanistan. "Lazima tulete chakula kwa familia. Ni lazima tuwaletee wakulima mbegu ili wavune. Tunapaswa kuleta huduma za afya nchi nzima. Na lazima tuwalinde wale wote wanaotaka kurejea Afghanistan, "alisema.

Tangu Taliban kuchukuwa madaraka, Afghanistan inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kifedha, mfumuko wa bei na ukosefu wa kiwango cha juu cha nafasi za kazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.