Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-JAMII

UNSC kuafikiana kuhusu kutumwa kwa misaada ya kibinadamu nchini Afghanistan

Huu ni mwanga wa matumaini kwa wananchi wa Afghanistan: maelewano yanakaribia kufikiwa ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuwezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu. Chini ya shinikizo kutoka China, Marekani imerekebisha rasimu ya azimio na kuachana na wazo la utaratibu wa "kesi-kwa-kesi" kwa ajili ya msaada huu ambao Waafghan wanauhitaji sana.

Raia wa Afghanistan wakiwa kwenye foleni kupokea pesa taslimu zinazotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, tarehe 3 Novemba 2021.
Raia wa Afghanistan wakiwa kwenye foleni kupokea pesa taslimu zinazotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, tarehe 3 Novemba 2021. AP - Bram Janssen
Matangazo ya kibiashara

Wengi wanahoji vipi kuhakikisha utoaji wa misaada ya kibinadamu bila kuukubali au kuhalalisha utawala wa Taliban? Vipi kutaidhinishwa benki, mashirika ya kiraia, taasisi za kimataifa kutoa msaada huu wakati viongozi wa nchi wako kwenye orodha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa? Ni suala hili tete ambalo jumuiya ya kimataifa inapaswa kutatua ili kuepuka janga la kibinadamu ambalo linaonekana kuwa mbaya zaidi.

Utaratibu wa kutoa huduma ya kwanza wakataliwa na China

Kama hatua ya kwanza, Umoja wa Mataifa ulitaka kuweka utaratibu wa msamaha wa kesi kwa kesi ili kuruhusu kutolewa kwa msaada huu. Utaratibu uliokataliwa na China ambayo, kwa msaada wa Urusi, ilikuwa imezuia rasimu ya azimio hilo. Washington hatimaye imekubali suala hili, na ikaondoa utaratibu huu kutoka kwa nakala yake. Hali hii inaonyesha matumaini ya kupitishwa haraka kwa msaada huu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kuna udharura kwa sababu nchi bado haijapata fedha zake zilizowekwa benki.

Uchumi wa Afghanistan umesimama, na mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yana wasiwasi kuhusu hatari ya kutokea njaa ikiwa hakuna kitakachofanyika kuwezesha kuwasili kwa haraka kwa misaada ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.