Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-JAMII

Afghanistan: Mji wa Kabul wakumbwa na mgogoro wa chakula

Miezi minne baada ya kuanguka kwa Kabul, Afghanistan inatumbukia katika mgogoro mkubwa wa chakula. Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya raia mmoja kati ya wawili wa Afghanistan atakabiliwa na uhaba wa chakula msimu huu wa baridi. Na msaada wa dharura wa dola milioni 280 uliotolewa Jumamosi hii, Desemba 11 na Benki ya Dunia hautoshi kuepusha njaa.

Tatizo sio usambazaji wa chakula. Mabanda yamejaa vyakula aina mbalimbali hususan kiwi, ndizi, parsley, maziwa na boga. Mgogoro unaripotiwa upande wa wateja ambao hawana uwezo wowote wa kununua chakula.
Tatizo sio usambazaji wa chakula. Mabanda yamejaa vyakula aina mbalimbali hususan kiwi, ndizi, parsley, maziwa na boga. Mgogoro unaripotiwa upande wa wateja ambao hawana uwezo wowote wa kununua chakula. Hoshang Hashimi AFP
Matangazo ya kibiashara

Tatizo sio usambazaji wa chakula. Mabanda yamejaa vyakula aina mbalimbali hususan kiwi, ndizi, parsley, maziwa na boga. Mgogoro unaripotiwa upande wa wateja ambao hawana uwezo wowote wa kununua chakula.

Kama mwanamke huyu aliyevalia hijabu ambaye amekimbilia kwa baadhi ya wanahabari wetu huko Kabul, akiwa amechanganyikiwa kabisa: “Nina watoto 9, hawajala kwa siku tatu… Nina nyumba inayokodiwa kwa pesa za Afghanistan 4,000 ( sawa na euro 36) kwa mwezi, hakuna chochote ninachoingiza... Je, ni lazima niuze watoto wangu? Mimi, nataka kuwauza, lakini hakuna anayeweza kuwanunua… Wana njaa sana… siwezi kuvumilia kuwaona hivyo… Ninapendelea kuuza mmoja ili kuwalishiza wengine. "

Shida kwa wauzaji pia

Maskini zaidi walipata misaada ya kibinadamu, lakini kwa mabadiliko ya utawala kila kitu kimebadilika. Na cha kushangaza ni kwamba, uhaba huo pia unawakumba wafanyabiashara. “Unajua, hakuna tunachoweza kufanya, amebaini mmoja wa wauza mchele na kunde. Hatuuzi chochote tena, katika miezi minne nilipoteza 90% ya mauzo yangu. Tunategemea wateja wetu, wanaohitaji kufanya kazi. Lakini hawalipwi tena ... Wangewezaje kuja na kununua chochote? "

Nani anyooshewe kidole cha lawama? “Kwa Waamarekani, ambao hawataki kutupatia pesa wanazozuiwa . Sio pesa za Taliban, ni pesa za Waafghanistan, "  amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.