Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-JAMII

Aghanistan: Benki ya Dunia yatoa msaada wa kibinadamu wa dola milioni 280

Benki ya Dunia ilitangaza Ijumaa hii, Desemba 10 msaada wa kibinadamu wa dola milioni 280 kwa Afghanistan kupitia ugawaji upya wa ufadhili kutoka kwa mfuko maalum wa ujenzi wa nchi (ARTF).

Benki ya Dunia inatangaza kwamba itatoa dola milioni 280 kwa Afghanistan.
Benki ya Dunia inatangaza kwamba itatoa dola milioni 280 kwa Afghanistan. Daniel SLIM AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo lilisitisha msaada kwa Kabul mwishoni mwa mwezi Agosti baada ya Taliban kurejea madarakani.

"Wafadhili [...] wa ARTF wameamua leo kukabidhi dola milioni 280 hadi mwishoni mwa mwezi Desemba 2021 kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, ​​​​na shirika la Mpango wa Chakula Duniani," imesema taarifa kutoka Benki ya Dunia.

"Uamuzi huu ni hatua ya kwanza katika kugawa upya fedha kutoka kmfuko wa ARTF ili kutoa misaada ya kibinadamu kwa raia wa Afghanistan katika wakati huu muhimu," inaongeza taasisi hiyo. ARTF ni hazina ya uaminifu ya wafadhili wengi ambayo huratibu usaidizi wa kimataifa ili kuboresha maisha ya mamilioni ya Waafghanistan. Benki ya Dunia inasimamia ARTF kwa niaba ya washirika wafadhili.

Ufadhili kwenda kwa Unicef ​​​​na WFP

Benki ya Dunia inahoji kuwa UNICEF na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, yamejiimarisha vyema nchini Afghanistan na yana uwezo wa kiusalama wa kutumia fedha hizi vizuri. Pesa hizo zitasaidia "kuziba mapengo ya ufadhili katika mipango yao iliyopo ya kutoa huduma za afya na lishe moja kwa moja kwa raia wa Afghanistan," inahoji taasisi hiyo.

Benki ya Dunia inataja kwamba Unicef ​​itapata dola Milioni 100 na WFP dola Milioni 180. Fedha hizi za ARTF zitawezesha Unicef ​​"kuwapatia watu milioni 12.5 huduma za kimsingi na muhimu za afya pamoja na chanjo ya watu milioni moja, wakati WFP itakuwa na uwezo wa kutoa msaada wa chakula kwa watu milioni 2.7 na karibu wanawake na watoto 840,000 kwa msaada wa lishe,” Benki ya Dunia imeongeza.

Raia wa Afghanistan wakumbwa na njaa

Wananchi wa Afghanistan wamekuwa wakikabiliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi, uhaba wa chakula na umaskini unaoongezeka tangu wapiganaji wa Taliban kuchukua mamlaka katikati ya mwezi Agosti. Nchi hiyo pia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa ukwasi, huku wafadhili wa kimataifa wakiwa wamesitisha msaada mkubwa ambao ulikuwa umeshikilia bajeti ya serikali kwa miaka ishirini.

Mojawapo ya changamoto ni jinsi ya kufikisha fedha kwa Afghanistan bila kuweka hatarini taasisi za fedha kwa vikwazo vya Marekani. Shida ambayo ambayo Benki ya Dunia inajaribu kukwepa kwa kugawa fedha kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.