Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-HAKI

Afghanistan: Taliban yapiga marufuku wanawake kusafiri peke yao

Taliban imetangaza Jumapili, Desemba 26 kwamba wanawake wanaotaka kusafiri masafa marefu lazima waambatane na mwanaume kutoka familia, ikiwa ni hatua ngumu za serikali licha ya ahadi zake za awali.

Wanawake wa Afghanistan sasa watalazimika kuandamana na mwanamume ikiwa wanataka kusafiri masafa marefu.
Wanawake wa Afghanistan sasa watalazimika kuandamana na mwanamume ikiwa wanataka kusafiri masafa marefu. AP - Felipe Dana
Matangazo ya kibiashara

Pendekezo hilo lililotolewa na Wizara ya Kukuza Utu wema na Kulinda uzalendo na ambalo lilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, pia linatoa wito kwa madereva kukubali kuwasafirisha wanawake kwenye magari yao iwapo tu watajisitiri kwa kuvaa “mavazi ya Kiislamu.

"Wanawake wanaosafiri zaidi ya maili 45 (kilomita 72) hawawezi kufanya safari hiyo ikiwa hawajaandamana na mtu wa karibu wa familia ambaye ni mwanaume," msemaji wa wizara hiyo Sadeq Akif Muhajir ameliambia shirika la habari la AFP.

Agizo hili linakuja wiki chache baada ya ombi la wizara kwa televisheni za Afghanistan kuacha kutangaza au kurusha "vipindi ambavyo wanawake hushiriki", na kuhakikisha kuwa waandishi wa habari wanawake wanavaa "hijabu ya Kiislamu".

Ahadi zilizovunjwa

Tangu waingie madarakani mwezi Agosti, Wataliban wameweka vikwazo mbalimbali kwa wanawake na wasichana, licha ya ahadi za awali kwamba utawala wao hautakuwa mkali kuliko wakati wa utawala wao wa kwanza (1996-2001).

Katika majimbo kadhaa, mamlaka za mitaa zimekubali kufungua tena shule za wasichana, ingawa wengi wao kote nchini bado hawawezi kuhudhuria.

Mapema mwezi Desemba, agizo kwa jina la kiongozi mkuu wa Taliban iliitaka serikali kutekeleza haki za wanawake, lakini amri hiyo haikutaja haki ya kupata elimu.

Wanaharakati wanatumai kwamba juhudi za Taliban kutaka kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa na kwa mara nyingine tena kupokea misaada inayohitajika kwa nchi hiyo - miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani - itawapeleea kufanya makubaliano.

Wakati wa utawala wao wa kwanza, Taliban walifanya kuwa ni lazima kwa wanawake kuvaa burqa. Waliweza tu kuondoka nyumbani kwao wakati wakiandamana na mwanamume na hawakuruhusiwa kufanya kazi na kusoma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.