Pata taarifa kuu
USALAMA-BAHARINI

Boti yazama kwenye pwani ya Madagascar, wahamiaji 22 wafariki

Wahamiaji 22 waliokuwa kwenye boti wakielekea katika kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte, katika Bahari ya Hindi, walifariki baada ya boti waliokuwemo kuzama siku ya Jumamosi kwenye pwani ya Madagascar, mamlaka ya baharini ya Madagascar imetangaza leo Jumatatu.

Polisi inazuia boti inayosafirisha wahamiaji kwenda Mayotte.
Polisi inazuia boti inayosafirisha wahamiaji kwenda Mayotte. AFP/Gendarmerie nationale
Matangazo ya kibiashara

"Watu arobaini na saba walisemekana kusafiri na boti hiyo kwa njia isiyo rasmii, wakitaka kufika Mayotte, lakini boti hiyo ilizama. 

Abiria 23 waliweza kuokolewa. Miili 22 ilipatikana", imesema mamlaka ya Bandari, Majini na Mito (APMF) katika taarifa kwa vyombo vya habari. Operesheni ya kutafuta miili mingine baada ya boti hiyo kuzama iliyoanza siku ya Jumamosi inaendelea, kulingana na mamlaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.