Pata taarifa kuu

Nchi mbalimbali barani Afrika zajiandaa kwa uchaguzi mnamo 2023

Mwaka wa 2023 utakuwa mwaka wa uchaguzi katika nchi nyingi za bara la Afrika. Benin inajiandaa kwa uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika Januari 8. Raia wa nchi nane wataitishwa kupiga kura za urais.

Carte du continent africain.
Carte du continent africain. © Montage RFI / Pierre Moussart
Matangazo ya kibiashara

Nchini Nigeria, nchi kubwa barani Afrika yenye wakazi zaidi ya milioni 200, inajiandaa kwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Februari 25 kwa uchaguzi wa rais na wabunge, na mwezi Machi kwa uchaguzi wa magavana na serikali za mitaa.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, ambaye amemaliza mihula miwili (2015-2019, 2019-2023), hatagombea. Kwa upande mwingine, Sierra Leone itafanya uchaguzi wa urais mwezi Juni, kwa upande wa Liberia uchaguzi wa urais utafanyika mwezi Oktoba na Madagascar mwezi Novemba, Julius Maada Bio, George Weah na Andry Rajoelina wanaomaliza muda wao wanaweza kugombea muhula wa pili.

Nchini Gabon, Katiba inamruhusu Rais Ali Bongo kugombea tena akipenda. Kwa upande wake, atakuwa anagombea muhula wa tatu wa miaka saba (2009-2016, 2016-2023).

"Nilisikia mwito wa wahusika wengi wa kisiasa na wapinzani wakiomba kuandaliwa kwa mkutano wa kufafanua misingi ya maandalizi ya uchaguzi (…). Ninawahakikishieni kuwa mkutano huu utafanyika haraka iwezekanavyo" , amesema Rais wa Gabon Ali Bongo.

Kwa upande mwingine Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pia inajiandaa kwa uchaguzi wa urais mwaka huu. Uchaguzi umepangwa rasmi kufanyika Desemba 20. Zoezi la kuandika wapiga kura limeanza rasmi lakini si kila mahali kwa sababu ya vurugu. Mkuu wa Nchi, Felix Tshisekedi, tayari ametangaza kuwa atawania tena katika uchaguzi huo. Alimrithi Joseph Kabila mapema 2019.

Nchini Zimbabwe, uchaguzi mkuu pia unatarajiwa mwaka 2023. Kwa upande mwingine, uchaguzi mkuu umeahirishwa rasmi nchini Sudan Kusini. Hautafanyika mwaka huu na kipindi cha mpito kimeongezwa kwa miaka miwili hadi 2024. Sudan Kusini haijawahi kuwa na uchaguzi wa rais tangu uhuru wake mwaka 2011. Mwishoni mwa 2013, vita vya wenyewe kwa wenyewe vya umwagaji damu vilizuka katika nchi hii, ambayo bado haijatulia hadi leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.