Pata taarifa kuu
HAKI-ELIMU

Madagascar: Elimu ya juu iko hatarini kulingana na chama cha waalimu watafiti

Elimu ya juu iko hatarini nchini Madagascar. Hii ni tahadhari iliyotolewa na Vyama vya Walimu na Watafiti wa Walimu (SECES) kwa viongozi wa serikali katika taarifa ndefu iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa facebook. Tamko linalofuata baraza la kitaifa la muungano mwishoni mwa juma. Uharibifu wa miundombinu, ukosefu wa njia, kutolipwa kwa wafanyakazi... chama kinashtumu serikali kwa kushindwa hatua.

Wanafunzi katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Antananarivo, Madagascar.
Wanafunzi katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Antananarivo, Madagascar. PHOTO / ALEXANDER JOE
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Antananarivo, Laetitia Bezain

"Elimu ya juu na utafiti wa kisayansi sio kati ya vipaumbele vya viongozi wa sasa", chama cha walimu watafiti kinasema katika taarifa yake.

Chamla hiki, ambacho kinawaleta pamoja wanachama wa vyuo vikuu vya majimbo sita ya Madagascar, kina wasiwasi hasa kuhusu kusimamishwa kwa kozi katika idara kadhaa za vyuo vikuu kutokana na kutolipwa kwa miaka minne ya wakandarasi. Walimu wasio watumishi wa umma ambao wanachangia kuziba pengu la wafanyakazi na ambao wanachukua asilimia 70 ya ualimu katika chuo kikuu.

Ukosefu wa rasilimali ambao pia umeathiri utafiti kwa miaka mingi. "Ruzuku zinazotolewa kwa vyuo vikuu na vituo vya utafiti ni ndogo sana na zimechelewa kutolewa", wanasema waalimu watafiti, ambao pia wanasikitishwa na idadi kubwa ya miundombinu "iliyoharibika" "Ikiwa Serikali haitachukua hatua, vyuo vikuu na vituo vya utafiti vitafunga, ” wanaonya.

Idara ya mawasilianokatika Wizara ya Elimu ya Juu inabaini kwamba inawasiliana mara kwa mara na chama hiki cha waalimu na kuongeza kuwa bajeti ya idara yake inategemea sheria ya fedha. Idara hii inaongeza kuwa katika suala la miundombinu, "kampasi tisa za vyuo vikuu zimejengwa katika mikoa kadhaa ya Madagascar. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.