Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Madagascar: Jean-Brunelle Razafitsiandraofa, kuwania katika uchaguzi wa urais

Jean-Brunelle Razafitsiandraofa, ni mgombea wa 11 kujitangaza rasmi katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais utakaofanyika Novemba 9 nchini Madagascar. Leo, Mbunge Jean-Brunelle Razafitsiandraofa ameamua kutetea na kuwakilisha "watu walio hatarini".

Mbunge wa Ikongo, Jean-Brunelle Razafintsiandraofa, na sasa mgombea wa uchaguzi wa rais wa 2023. Alichaguliwa chini ya bendera ya IRD, chama cha rais.
Mbunge wa Ikongo, Jean-Brunelle Razafintsiandraofa, na sasa mgombea wa uchaguzi wa rais wa 2023. Alichaguliwa chini ya bendera ya IRD, chama cha rais. © Sarah Tétaud/RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Antananarivo, Sarah Tétaud

"Sikuweza tena kukaa kimya," anasema mbunge wa mkoa wa Ikongo na Naibu spika wa Bunge la kitaifa. Iwapo atachaguliwa, Jean-Brunelle Razafitsiandraofa anakusudia kutetea ardhi “katika maana nzuri na pana ya neno hilo” (wakulima, urithi, mila) lakini pia raia wa Madagascar, leo “wanadharauliwa” anasema, “wamedidimizwa na kutekwa nyara na kundi la watu wadogo wanaoshikilia mamlaka. Watu wanasema "wasomi", lakini sio wasomi. Ni kundi la watu wadogo wanaofanya uhalifu tu! Hai ya nchi iko kwenye mstari mwekundu.”

Utapiamlo, njaa, mauaji ya watu wengi: ni hali hizi za dharura zinazorudiwa zilizorekodiwa katika wilaya yake kusini-mashariki mwa kisiwa hicho ambazo zilimshawishi mbuge huu aliyechaguliwa kugombea kwenye kiti cha urais. Mbunge huyo aliyechaguliwa chini ya bendera ya IRD, chama cha rais, ameendelea kuipa kambi yake wakati mgumu katika miezi ya hivi karibuni. Misimamo yake nje ya mawazo ya chama na maneno yake mazito ya kukemea mara kwa mara hali mbaya ya kiafya ya binadamu na hali katika mkoa wake wa Ikongo, kumemfanya aheshimiwe nchini.

“Ninawaalika mkague na kuchukua hatua. Chini ya mabunge mawili yanayounga mkono utawala, wilaya yangu ya uchaguzi ilipata nini katika masuala ya maendeleo na miundombinu? Hakuna kitu! Kama "zawabu", wenzangu waliuawa kwa risasi za moto mnamo Agosti 29 wakati hawakuwa wamevuka mstari mwekundu kwenye lango la kambi ya jeshi. Bila uchunguzi. Tuko katika jamhuri gani?! "

"Sitaweza kuendelea na wagombea ambao wana na watatumia pesa nyingi. Lakini nitaishi nao. "

Akifahamu uwezo wake wa kifedha, ambao ni mdogo zaidi kuliko wale wa baadhi ya washindani wake, mbunge Jean-Brunelle Razafitsiandraofa anategemea kuona mtazamo wa wapiga kura na nia yao ya mabadiliko.

Mkuu wa zamani wa mamlaka ya uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ivato napeperusha leo bendera ya chama cha "Antoko Politika Madio", kihalisi "Chama Safi cha Siasa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.