Pata taarifa kuu

Madagascar: Rais Andry Rajoelina anaoongoza kwa mujibu wa matokeo ya awali

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, amechukuwa uongozi wa mapema kwenye uchaguzi uliofanyika juma lililopita, akiongoza kwa siliamia 62.4.

Uchaguzi wa  Madagascar
Rais anayeondoka madarakani Andry Rajoelina wakati akihotubia wapiga kura nchiniu Madagascar kuelekea uchaguzi mkuu REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Asilimia 37 ya kura zote zikiwa tayari zimehesabiwa rais Rajoelina anaongoza kura hizo akifuatwa kwa umbali na mgombea mwingine Siteny Randria-nasolo-niaiko kwa asilimia 12.2 naye rais wa zamani Marc Ravalomanana, akifunga tatu bora kwa asilimia 11.2%.

Tume ya uchaguzi nchini Madagascar imesema asilimia 43 ya raia  wamelijitokeza kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Viongozi kadhaa wa upinzani wakidai hilo limechangiwa na wao kuwataka raia kutojitokeza kwa misingi kuwa kulikuwa na njama ya wizi wa kura.

Zaidi ya wagombea 10 wa upinzani kati ya 12, walisusia uchaguzi huo, baada ya kushindwa kuzuia rais Rajoelina kuwania urais kwa misingi ya kwamba ana uraia picha, akiwa ni pamoja na uraia wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.